[wanabidii] NIMEFUNGUA OFISI YA USHAURI WA BIASHARA SINZA KWA REMI

Thursday, December 12, 2013


Napenda kuwafahamisha kwamba kuanzia tarehe 1/12/2013 nimeanzisha kampuni ya ushauri ijulikanayo kwa jina la; CPM Business Consultants.
Kampuni hiyo inajishughulisha na kutoa ushauri wa biahshara kwa Wafanyabiashara wadogo wa kati na wakubwa. Pia inatoa ushauri kwa uendeshaji wa Taasisi za Serikali, Mashirika ya Umma na Mashirika yasiyo ya kiserikali NGO. Washauri wetu wana ujuzi wa ngazi za shahada za uongozi na uzoefu wa muda mrefu katika kazi za ushauri na uendeshaji wa asasi mbali mbali ikiwa ni pamoja na asasi za kifedha kama vile SACCOS na VICOBA. Ofisi yetu iko Sinza kwa Remi.Kwa mawasiliano piga simu namba 0784394701 au 255755394701 tuma barua pepe cnazi2002@yahoo.com Nyote mnakaribishwa.

MALENGO YA KAMPUNI 
Malengo ya kampuni ni kutoa huduma bora za ushauri kwa Wafanyabiashara wadogo wa kati na wakubwa,Taasisi za Serikali, Mashirika ya umma, SACCOS na Asasi zisizo za kiserikali NGO ili ziweze kuendesha shughuli zao kwa ufanisi. 

DIRA YA KAMPUNI
Sisi tunaamini kwamba matatizo yanayozuia maendeleo ya Wajasiriamali Tanzania ni pamoja na ukosefu wa mitaji na elimu ya biashara,hivyo lengo letu ni kuhakikisha tunatoa elimu ya biashara na uendeshaji ili biashara na asasi ziweze kuendeshwa kwa ufanisi. 

BIDHAA ZETU
1.Kutoa ushauri wa biashara kwa Wafanyabiashara wadogo wa kati na wakubwa, 
2.Kuandaa michanganuuo kwa ajili ya kuomba mikopo benki na misaada kutoka kwa wafadhili.
3.Kutoa mafunzo ya Ujasiriamali kwa wafanyabiashara.
4.Kuandaa mifumo ya utunzaji wa mahesabu na kuweka mifumo ya Kompyuta kwenye utunzaji wa hesabu.
5.Kuandaa katiba za vyama na nyaraka za uandikishaji wa makampuni.
6.Kuandaa nyaraka za Tenda.
7.Kutoa ushauri kwa SACCOS ili ziendeshwe kwa ufanisi. 
8.Kutoa ushauri kwa Asasi zisizo za kiserikali NGO ili ziweze kuendesha shughuli zao kwa ufanisi.
9.Kutunga vitabu za biashara ili kuwafikia wafanyabiashara wengi zaidi.
10.Kutoa ushauri nasaha na semina kwa wanafunzi.
11. Kutoa ushauri kwa taasisi za Serikali na Mashirika ya umma.

MIPANGO YA BAADAYE
Kuimarisha biashara ili tuweze kuenea mikoa yote ya Tanzania.

CHARLES P.M.NAZI
MKURUGENZI MTENDAJI
CPM BUSINESS CONSULTANTS.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments