CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) CHADEMA JIMBO LA TEMEKE
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
YAH:KUPINGA KAULI YA MWENYEKITI WA JIMBO LA TEMEKE NDUGU JOSEPH PATRICK YOHANA ALIOITOA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ndugu wanahabari sisi viongozi na wanachama wa Chadema Temeke tunapinga kwa kauli moja tamko liliotolewa na mwenyekiti wa Chadema jimbo la Temeke lakupinga maamuzi ya kamati kuu na kudharau agizo la katibu mkuu wa chama Dr Wilbrod salaa ya kuwa mijadala yote inayohusu uamuzi wa kamati kuu kuwavua uongozi Zitto na wenzake imefungwa
Hii inadhihirisha kuwa mwenyekiti wa jimbo la Temeke hana utovu wa nidhamu kwa chama na viongozi wake wajuu
Kauli ambazo bwana joseph yona amezitowa katika magazeti ya 29-11-2013 mwananchi,Rai,Mtanzani na majira ni kama zifwatazo.
1. Kupinga vikali maamuzi ya kamati kuu kwa niaba ya wanachama wote wa Jimbo la temeke
2. Kuziita operation za chama yani vuguvugu la mabadiliko M4C ni uhaini
3. Kusema kuwa kila wakati chama kinapoelekea kwenye uchaguzi za ndani Viongozi wanaanzisha migogoro
Kwa kufanya haya yote bwana joseph yohna Patrick avunja katiba kifungu namba 10.1(viii,ix,x)
Msimamo wa chama Temeke
Sisi kama wanachama na viongozi wa jimbo la Temeke tuna towa tamko rasmi kwamba tunaunga mkono uhamuzi wa kamati kuuu, pia tuna mtaka bwana Joseph Yohna Patrick afute kauli yake kwa vyombo vya habari la sivyo tutamchukulia hatua za kinidhamu
Taarifa hii imeandaliwa na wanachama na viongozi wa M4C Temeke
Asante
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments