[wanabidii] UPOTOSHAJI WA ZIARA YA MWENYEKITI TAIFA CHADEMA KANDA YA ZIWA MASHARIKI.

Thursday, November 07, 2013
UPOTOSHAJI MKUBWA WA ZIARA YA MWENYEKITI TAIFA CHADEMA(Mbowe) KANDA YA ZIWA MASHARIKI.


Kwa karibia wiki sasa mitandao ya kijamii kumekuwa kukifanyika juhudi kubwa ya kupotosha lengo na shabaha ya ziara ya Mwenyikiti Mbowe. Kume kuwa na genge la watu wakiandika/wakisema Mbowe kaja kanda ya ziwa mashariki kwa lengo la kuweka watu wenyemtazamo wake na kuwang'oa wenyemlengo wa kumshabikia Zito Kabwe.


Natumia fursa hii kusema ukweli wa kilichotokea ziwa masahariki yaani mikoa ya Mara, Shinyanga na Simiyu. Pia yapaswa ieleweke maelezo haya ni observation yangu na sio ya CHAMA ijapokuwa mimi ni kiongozi wa CHAMA nimejaribu kujizuia nisijibu kelele hizi na nisubiri kikao kitoe tamko kikatiba lakini naona nawajibika kulisemea hili. Nasema hili kwa haki na ukweli kabisa bila kujali madhila yoyote.

Kwanza ujio wa Mwenyekiti (MBOWE) ni ombi la uongozi wa kanda na tulimwomba Mwenyekiti aje kwenye kanda yetu kuweka mambo sawa ya kiuongozi na ombi hilo liliombwa makao makuu ya chama ana kwa ana na kwa taarifa ya utekelezaji ya kanda (mimi ndo nilosoma taarifa hiyo). Na baada ya ombi letu Mwenyekiti na wasaidizi wake wakatupangia tarehe ya kuja na ikawa 1,2 na 3 november hii.

Shabaha ya Ziara ya mwenyekiti katika kanda hii ya ziwa mashariki ilikua:………..
Ø Kuhamasisha ushiriki wa wadau(professionals and middle classes) katika uungaji mkono shughuli za chama ndani ya kanda. Na hii ndiyo ilisababisha mikutano/vikao kufanyikia Kahama, Shinyanga na Mara, miji hii ilionekana ndo ina wadau potential zaidi isingekuwa sababu hii kikao kimoja kingefanyika kati ya Bariadi au Maswa badala ya kahama.


Ø Kuunda uongozi wa kanda, ieleweke uongozi wa kanda yetu haukuwepo zaidi kulikuwa na watu wa kukaimu nafasi mbalimbali. Na katika kutekeleza hili hatimaye uchaguzi ulifanyika shinyanga mjini katika ukumbi wa Carena hotel na maokeo yakawa..
· Mhe kasurumbayi, s. MB alipata kura 85.
· Mhe Madata B, alipata kura 71
· Mhe Rev Mayalla alipata kura 18
· Mhe Chiliko H,D. alipata kula 6
· Mhe Kitarama alipata kura 4.
Na maamuzi ikawa Mhe kasurumbayi ameshinda.

Ø Kuunda uongozi wa Muda wa mkoa wa Simiyu. Zingatia Simiyu ni mkoa mpya umeundwa mwaka 2012 hivyo haukuwa na uongozi wa chama. Hili lilfanyika kwa demokrasia kabisa na waliopiga kura ni wajumbe wa vikao vyva mashauriano vya mikoa husika tu. Na mihasari ipo.( simiyu mkt alichagulia Eng Mshuda Wilson.)

Ø Kuboresha uongozi wa ngazi ya mikoa kwa mikoa ya Mara na Shinyanga. Kwa mkoa wa shinyanga nafasi ya mkt wa mkoa iko wazi tangu afariki Marehemu Shelembi lakini mamuzi hayakufanyika kwa sababu wajumbe wa kikatiba hawakufikia akidi. Kwa mkoa wa Mara katibu wa chama alifukuzwa na kuhamia CCM tangu mwaka 2010 na baadhi ya ziongozi walikuwa hoi kiasi kwamba hata vikao havikuwa vikifanyika. Katika kikao cha mashauriano(mkoa Mara) wajumbe wakaazimia uongozi wote uzunjwe na wakaweka uongozi wa muda.
Baada ya maelezo hayo marefu na ieleweke hivyo vinginevyo ni uzushi wa kawaida wa CCM.

Na Frank Kubwera 0764363651
06/11/2013

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments