[wanabidii] Taarifa ya Mkemia Mkuu kupitia Polisi: Utambuzi wa mihadarati iliyokutwa katika maiti

Tuesday, November 19, 2013

NYONGEZA YA TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI "PRESS RELEASE" TAREHE 18.11. 2013.

WILAYA YA MBEYA MJINI – UTAMBUZI WA MADAWA YA KULEVYA YALIYOPATIKANA KATIKA MWILI WA MAREHEMU KASSIM S/O SAID MBOYA.


·         MNAMO TAREHE 15.11.2013 MAJIRA YA SAA 17:00HRS HUKO KATIKA OFISI YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI JIJINI DSM ULIFANYIKA UCHUNGUZI WA KITAALAM KUHUSIANA NA MADAWA YADHANIWAYO KUWA YA KULEVYA YALIYOKUTWA KATIKA MWILI WA MAREHEMU KASSIM S/O SAID MBOYA.

·         MADAWA HAYO YALIPOPIMWA AWALI YAKIWA KATIKA MUUNDO WA PIPI ZIPATAZO 65 NA MOJA IKIWA IMEPASUKA ZILIZOVINGIRISHWA KWA KUTUMIANYLON MAALUM YALIKUWA NA UZITO WA KILO 1 NA GRAM 140. HATA HIVYO KATIKA UCHUNGUZI HUO MADAWA HAYO YALIBAINIKA KUWA  NA UZITO WA GRAM 972. 85 IKIWA NI BAADA YA 
KUYATOA MADAWA HAYO KATIKA NYLON MAALUM HIVYO UZITO WA NYLON MAALUM PEKEE NI GRAM 167.15 NA YALIBAINIKA KUWA NI AINA YA HEROINE.

§         AWALI MNAMO TAREHE 07.11.2013 MAJIRA YA SAA 11: 00HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. KASSIM S/O SAIDIMBOYA, ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO.

§         MAREHEMU ALIKUWA ANASAFIRI KUTOKA DSMKUELEKEA LILONGWE NCHINI MALAWI AKIWA KATIKAM BASI LA TAQWA LENYE NAMBA ZA USAJIRIT.319 BLZ AINA YA NISSAN AKIWA NA HATI YA KUSAFIRIA NAMBA – AB 051010 PIA AKIWA NA BEGI DOGO LENYE SURUALI MOJA AINA YA JEANS, T-SHIRT MOJA NYEUSI, RABA JOZI MOJA RANGI NYEKUNDU, MKATE MMOJA, MKOBA MDOGO WA KIUNONI, VACCINATION CARD MBILI ZA KINGA YA UGONJWA WA MANJANO, RAND MBILI SARAFU ZA AFRIKA YA KUSINI NA MIFUKO SITA [06] YA RAMBO RANGI NYEUSI.

§          BASI HILO BAADA YA  KUFIKA MPAKANI KASUMULU NA ABIRIA KUSHUKA KUTOKA KWENYE GARI HILO NA KUANZA KUFANYA TARATIBU ZA  KUVUKA MPAKA KUINGIA NCHINI MALAWI, MAREHEMU ALIBAKI NDANI YA  GARI HUKU HALI YAKE YA  KIAFYA IKIZIDI KUDHOOFIKA. WAHUSIKA WA GARI WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI AMBAPO MAREHEMU ALICHUKULIWA NA KUKIMBIZWA HOSPITALI YA  WILAYA YA  KYELA KWA MATIBABU. HATA HIVYO KABLA HAJAPATA MATIBABU ALIFARIKI DUNIA. MWILI WA MAREHEMU ULISAFIRISHWA HADI HOSPITALI YA  RUFAA MBEYA NA KUFANYIWA UPASUAJI AMBAPO ZILIPATIKANA PIPI 65 TUMBONI.

§         MNAMO TAREHE 11.11.2013 MAJIRA YA  SAA 14:10HRS HUKO KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI KATIKA HOSPITALI YA  RUFAA MBEYA JIJI NA MKOA WA MBEYA. JESHI LA POLISI LILIWAKABIDHI MWILI WA MAREHEMU KASSIM S/O SAIDI MBOYANDUGU ZAKE WAWILI AMBAO NI BABA WA MAREHEMU AITWAE SAID S/O ATHUMANI MBOYA, MIAKA 60, MPOGORO, MKULIMA, MKAZI WA MWANANYAMALA – MCHANGANI – DSM NA MDOGO WAKE NA MAREHEMU AITWAE HASSAN S/O SAID MBOYA, MIAKA 28, MPOGORO, TINGO KAMPUNI YA  MOHAMED ENTERPRISES DSM, MKAZI WA MWANANYAMALA MCHANGANI –DSM. BAADA YA UTAMBUZI NDUGU HAO WA MAREHEMU WAMEMUELEZEA MAREHEMU NDUGU YAO KUWA  ALIKUWA ANAITWA KASSIM S/O SAIDI MBOYA, MIAKA 36, MPOGORO, MKULIMA, MKAZI WA MWANANYAMALA-MCHANGANI –DSM.

§         KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA  WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI  KINYUME CHA SHERIA, NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI PIA INAPUNGUZA NGUVU KAZI YA TAIFA.


[DIWANI ATHUMANI- ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments