Nianze kwa kuwasalimu nyote ambao kwa namna moja au nyingine, na kwa nyakati tofauti tofauti mmendelea kuwa wadau wa maendeleo ya mkoa wa Singida. Nia yenu ya dhati ya kushiriki moja kwa moja katika kuusemea Mkoa wa Singida kwa namna yeyote, ipo siku itakuja na matokeo makubwa ya heshima iliyotukuka kwa Mkoa wa Singida, hata kama sisi sote na kizazi chetu hatutakuwepo.
Niwaombe radhi pia wale ambao hamtaweza kusoma ujumbe huu hadi mwisho, ila kwa watakaoweza twende pamoja kituo kwa kituo.
Katika harakati zozote zile za kutafuta maendeleo ya mahali Fulani, silaha ya kwanza huwa ni utambulisho wa wazi wa wanaharakati. Hakuna anayeweza kudai anapigania maendeleo ya Tanzania huku akiogopa kujitambulisha kuwa yeye ni Mtanzania, labda kama hamaanishi anachokipigania. Ninapata moyo kwa kuwa leo hii tofauti na miaka kumi iliyopita, si aibu tena kwa mtu kusema anatoka mkoa wa Singida. Kwa wale wenye kumbu kumbu nzuri hawatasita kuniunga mkono katika hili.
Nilipojiunga na masomo ya kidato cha tano, nilipata bahati ya kuchaguliwa kuwa Raisi wa serikali ya wanafunzi. Kwa bahati mbaya au nzuri, nilikuwa katika mkoa wa watu wenye uzalendo wa hali ya juu kwa mkoa wao, tena wenye uwezo mkubwa wa kiuongozi. Harakati zangu za kuitafuta nafasi hiyo haikuwa ngumu kabla watu hawajajua natoka mkoa gani. Kwa bahati mbaya, siku moja waliniuliza natoka ukoo gani katika kabila lao. Mimi sikusita kukiri kuwa natoka mkoa wa Singida, na hapo sasa ndipo nilipojua maana halisi ya uzalendo.
Nilipingwa hadharani kwa kigezo cha pahala nnapotoka. Wapo waliokuja na hoja dhaifu kuwa wamepata habari kuwa wanaotoka mkoa wa Singida wengi waliwahi kuugua Unyafuzi, kwashakoo na mengine ya namna hiyo hivyo walikuwa na shaka kuwa sitafanya vema katika nafasi ile. Kwa kweli nilikata tamaa, lakini nikatiwa Nguvu na ukweli kuwa uwezo nilikuwa nao. Niliwathibitishia hilo kwa mikakati niliyoibainisha tangu mwanzo kuwa uwezo wa kuwatumikia ninao, na walikubaliana name pale nilipomburuza vibaya "mwenzao mmoja".
Ndugu zangu, miaka kadhaa iliyopita isingekuwa rahisi kwa mtu kujitambulisha kuwa anatoka Singida. Mtu angekuwa tayari kubaki na maumivu moyoni anapowakuta watu wakiujadili mkoa wa Singida kwa mabaya, tena wakati mwingine nae akaongeza neno kuukashifu mkoa wa Singida na watu wake huku akiijitambulisha kuwa ni Mzaramo wa Mzizima au Mkwere wa Bagamoyo. Hata nilipofika chuo, haikuwa bado kazi rahisi kuwaunganisha wanafunzi watokao Singida kwa kuwa sio wote walikuwa tayari kukiri kuwa wanatoka mkoa wa Singida.
Hali haiko hivyo tena leo. Watu wanaamka na wanakiri ukweli waliouvumilia kwa muda mrefu. Leo sio ajabu kusikia watu wakisalimiana "habariki".., "njija, mufanga?' tena wakiwa mtaa Kongo pale Kariakoo. Tena wengine utawasikia wakifunguka "ulaileani".., "Iiiza.., mupanga?" pembeni ya Millennium Tower pale Kijitonyama, Vijana wa siku hizi wanasema KIROHO SAFI KABISA. Huku ndipo tulipokuwa tunataka kwenda, na ndio hasa matarajio yetu.
Hata hivyo, nia yetu ya dhati sio kukua na kupanuka kwa makabila yetu. Narudia tena kwa msisitizo, NIA YETU YA DHATI SIO KUKUA NA KUPANUKA KWA MAKABILA YETU. Tukiaanza harakati za kukuza makabila yetu sio vibaya pia, na huo ni uzalendo. Ila utakuwa ni Uzalendo wa KIWENDAWAZIMU. Kwanza, humu ndani tutaunda makundi makubwa matatu. Kundi la kwanza litajiita "WAZAWA", na hawa watajivunia zaidi kuzaliwa mkoa wa Singida, tena kwa asili kabisa, na sina shaka, wanyisanzu, Wanyaturu na wanyiramba wote tutasimama upande huu. Kundi la pili litaitwa "WAKUJA". Wale wote waliohamia mkoa wa Singida kutoka mikoa mingine watasimama upande huu. Kundi la mwisho ni wale wapiti njia tu, walikuja Singida mara moja wakapapenda ila wameshahamia pahala pengine. Kumbe utakuwa ni mtifuano kati ya waliozaliwa Singida kwa maana ya wenye asili halisi ya mkoa wa Singida, na wale waliohamia Mkoa wa Singida. Kimantiki, kundi la wazawa litakuwa na Nguvu zaidi kuliko makundi mengine.
Ubaguzi ni ubaguzi tu, hali haitakuwa shwari hata kwa wale wazawa. Huko nako watakapokaa pamoja, watatambua kuwa wao si wamoja, Wanyaturu watajiita SISI WANYATURU na wanyiramba watajiita SISI WANYIRAMBA. Ikifikia hapo, habari haitakuwa MKOA WA SINGIDA TENA, habari itakuwa KABILA HILI au KABILA LILE. Tukubali ama tukatae, hali ikifika huko, hakuna atakayeyatafuta maendeleo ya Mkoa tena, kila mtu atasimama kwa kabila lake.
Niwakumbushe kitu kimoja. Kuzaliwa ukiwa wa kabila Fulani ni AJALI ya kihistoria tu. Hakuna aliyepeleka maombi kwa Mungu ili azaliwe akiwa Mnyaturu, au mchaga, au Msukuma, au Mkwere, au Mndengereko, au Mnyaswa, au Mkwavi, au Mnyakyusa au Mpare. Haya yametokea kama ajali tu, na hayapaswi kuwa mambo ya kushabikia. Kuna mnyaturu leo anatamani angezaliwa akiwa Mchaga, na kuna Mchaga anatamani angekuwa anaitwa HANGO.
Lakini swala la kuamua eneo la kuishi linafanyika kwa kuamua. Kuna wanyaturu ambao leo hii wameenda kuishi Mwanza, NA HAWATAKI KURUDI SINGIDA. Kuna wasukuma ambao wamekuja kuishi Singida, NA HAWATAKI KURUDI MWANZA. Huu ndio utashi, haya ndio maamuzi.
Harakati za kuujenga Mkoa wa Singida zitumike kama jukwaa la kuwaunganisha wote wenye kupenda maendeleo ya Mkoa wa Singida, wawe Wanyaturu, Waarabu, Wandengereko, Wakara, wamasai, wachaga, wairaki, wameru, wasandawe, warangi na makabila yote. Hawa wameamua kwa utashi wao kuupenda mkoa wa Singida. Tunapoanza kujitenga kwa kutangaza ukabila, tunawavunja moyo na wanarudi nyuma. HATUTAFIKA MBALI.
Kuna Mchaga leo ameshasahau machalari, mtori na mbege, yeye na Ikhonda, mtama kwa mtukuru. Kuna Mmasai leo ameshasahau kuchunga, yeye analima alizeti kule Ikhanoda. Kuna Mpare leo ameshasahau dengelua na Makande au ugali kwa picha ya samaki, yeye na ndalu tu kule Ulemo. Kuna Mngoni leo kasahau kucheza malivata ya kwao, yeye na Ilanda tu. JUU YA YOTE, KUNA MNYIRAMBA LEO HAJUI KUSAGA NDALU, YEYE ANAJUA KUKOBOA MPUNGA TU. NA KUNA MNYATURU LEO KASAHAU MLENDA, YEYE NA PIZZA KWA BAGA TU. Hivi kati ya hawa wote, nani anateingizwa kwenye mapambano ya maendeleo ya mkoa wa Singida?
Kuna dada wa kinyaturu nnaishi nae nyumba moja hapa DSM, na alizaliwa Siuyu pale akiwa anaitwa Nyamoka Ipini, ila leo anajiita MANKA SHAYO a.k.a Manker The Gwan. Ukitaka akuharibie siku we msalimie Kinyaturu, Hakyamungu utajuta siku hiyo.Ukitaka akupe hela ya vocher we mwambie "Shimboni nashicha".., hapo mtaelewana. Huyu yupo Facebook pia, na anayetaka amtafute.
Nimalizie porojo zangu kwa kuwakumbusha kuwa, misingi ya ukabila ni dhaifu sana, haijawahi kutumika popote kujenga kitu. Hata mahusiano na kimapenzi hayawezi kujengwa juu ya misingi ya kikabila, YATAKUFA TU. Misingi ya undugu ni bora na mara zote inapotumika, imekuja na mafanikio makubwa. Wananchi wa Singida tusikubali kuunganishwa kwa Unyiramba, Unyaturu, Urangi, Unyisanzu wala ubargaigi wetu. Tuunganishwe na undugu na upendo wetu kwa Mkoa wa Singida.
HAKUNA ATAKAYEMUHESHIMU MNYATURU AISHIYE UFARANSA KAMA MKOA WA SINGIDA UKO CHINI KIMAENDELEO. LAKINI DUNIA NZIMA ITAMUHESHIMU MNYATURU, MNYIRAMBA, MCHAGA, MRANGI, MGOGO AU MSUKUMA AISHIYE SINGIDA KAMA MKOA WA SINGIDA UMEENDELEA.
Kila la heri.
ZEE LA KALE
0763 305605
-- Niwaombe radhi pia wale ambao hamtaweza kusoma ujumbe huu hadi mwisho, ila kwa watakaoweza twende pamoja kituo kwa kituo.

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments