Hatimaye Tunasoma ripoti ya Ujasusi aliofanyiwa Zitto wakati akipanga kukihujumu chama chake.
Mimi si jasusi wa CHADEMA wala si mwanachama wa CHADEMA. Ni mwana CCM lakini ni Mtanzania zaidi. Hii iko wazi katika michango yangu. Licha ya kutokuwa jasusi wa CHADEMA dalili za uasi wa Zitto ulikuwa unaonekana wazi. Wakati mwingine nilikuwa nawashangaa wasiouona na wakati mwingine nilikuwa nawashangaa wanaouonyesha bila kukusudia.
Hebu jiulize Zitto wa hoja ya Buzwagi ndiye huyu tunayemuana siku hizi?
Jiulize tena-Humu jukwaani na nje magazetini watu gani walikuwa wanasema nini juu ya Zitto? WanaCCM walikuwa wanamsemaje Zitto? na mengine mengi.
Kosa la Majasusi wa CHADEMA:
Mara kadhaa nimeandika humu kuwa CHADEMA inafanya vyema kwenda na Zitto hivihivi bila kumgusa.
Ningekuwa naishauri CHADEMA ningewaambia wamwite wamuonyeshe ripoti ya Ujasusi halafu wanyamaze. Asingeweza kufanya zaidi.
Au wangeweza kuitoa hadharani halafu wakanyamaza.
Kitendo cha kumuondolea madaraka na wajibu wake ni dalili kuwa CHADEMA haijawasoma watanzania. Kinachotarajiwa sasa ambacho CHADEMA ilistahili kukiepuka ni kuwagawa wanachama kwa kutenda walichotenda. Sio wanachama wote na waTanzania wote walikuwa wamemuelewa ZITTO. Na sio watanzania wote watakaoelewa maana ya ripoti ya Ujasusi. Bado kuna upofu. Ngoja 2015 ije. Bado kuna watanzania wanashabikia rangi za vyama sio sera.
Kama CHADEMA wangemuonyesha zitto wanavyomuelewa au wakaweka ripoti hadharani wakamuacha angefanya kosa yeye. Sasa wamefanya wao. Lazima mtikisiko utatokea na utatokea wakati mbaya. Karibu na uchaguzi wa Chama na karibu na uchaguzi Mkuu. 2014 na 2015 si mbali sana. Wanaojadili watavhusisha kitendo cha CHADEMA na uchaguzi. Hii sio afya kwa CHADEMA.
Nawatakia waTanzania kuisaidia Taasisi yao hii muhimu kabla ya Uchaguzi ili uweze kwenda kwa haki. Ikiwa matatizoni watanzania watachagua kitakachokuwepo.
Haifai
0 Comments