[wanabidii] RAIS WA 2015 AANDIKE TUJUE FIKRA ZAKE

Saturday, November 16, 2013
Mpaka sasa orodha ya wagombea urais kupitia Chama tawala na upinzani yanazidi kuongezeka. Laiti wangekuwamwagombea makini wa kutosha tungekuwa tunasoma mawazo mengi kuhusu fikra zao kwa,changamoto zinazolikabili taifa katika nyanya mbalimbali na umasikini kwa ujumla wake. Kiongozi kuandika inakufanya utabirike na umma ukupambanue unawaza nini kuhusu masuala mbalimbali muhimu ya ndani na nje ya nchi; afrika mashariki, afrika na dunia kwa ujumla. Ni bahati mbaya sana kwamba rais pekee alokuwa akiandika na Mwl Nyerere. Walio salia wote ni kubahatisha na badae tunakuja kulaumiana kwasababu tunachagua mtu tusiemjua vizuri. Hivi 2015 inakaribia, kuna karibu watu10 wameonesha nia ya kuutaka urais kwa namna mbalimbali. Lakn wote hakuna aliyewahi kuandika kitabu kuhusu mawazo yake katika masuala mbalimbali ya binadamu na maendeleo yake Tanzania na namna anavyofikiri kuhusu changamoto.mpaka tutafika mwaka wa uchaguzi bado raia wanashindwa kumtofautisha slaa, lowasa, membe, sitta na lipumba kuhusu masuala muhimu yanayohusu nchi ndani na nje. Lakn Kama watu hawa wangekuwa wanandika tungeshaaanza kuwatofautisha japo kwa kusoma vitabu vyao.ni. Aibu sana kwa taifa Lenye nusu karne bado tunabaki na mpambano wa wagombea urais kwa mipasho badala ya fikra.

Source : David Kafulila

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments