Watanzania tunashangaa hizi pembe za ndovu zinazokamatwa kila kukicha zinatoka wapi? Ukizitazama zinaonekana sio mpya ni za zamani sana. Ushauri kwa inteligensia wetu ni kwamba, kuna nyumba inaitwa Ivory House ipo hapa mjini. Humo zimehifathiwa pembe ambazo ziliwekwa zamani na serikali baada ya biashara ya pembe kuzuiwa duniani. kama mna kumbukumbu Kenya walizichoma za kwao lakini Tanzania walikataa.
Sasa wasiwasi wangu ni kwamba hizi ndizo zinatolewa huko kinyemela na wajanja na kubadilishia huko nyingine feki wahusika wenye uchungu na nchi hii naomba wachunguze kama pembe zilizopo Ivory House ni za kweli au feki? hapo ukweli utajulikana. Msishangae ndani ya nyumba hiyo mkakuta vipande vya miti au pembe za ng'ombe badala ya pembe za ndovu .USHAURI WA BURE

0 Comments