[wanabidii] NAJIULIZA NI NANI BOSS WA WABUNGE?

Wednesday, November 06, 2013
Najiuliza swali hili kwa kuwa jana nilikuwa naangalia TV wakati mjadala wa fao la kujitoa hususan kwa  mfuko wa jamii wa GEPF ulipokuwa unajadiliwa. Viti vya wabunge vilikuwa vitupu karibu asilimia 80 ya wabunge hawakuwepo bungeni. Najiuliza hivi ubunge si kazi kama kazi nyingine? Inakuwaje wanalipwa mishahara tena minono na hawafanyi kazi yoyote? Na huyo Bosi wao hawa wabunge yuko wapi? Haoni? kwanza ni Spika,Serikali au Wananchi? Chukulia wewe unapofanya kazi usipohudhuria kazini kwa siku tatu mfululizo achilia mbali kwamba hutalipwa mshahara bali pia utafukuzwa kazi. Sasa inakuwaje kwa wabunge? Hawafiki kazini halafu wanalipwa mishahara na posho na hakuna anaewawajibisha. Nchi itaenda hivi mpaka lini? Naomba wabunge wawajibishwe wahudhurie vikao vya bunge mwanzo hadi mwisho maana ndio kazi yao wanyolipiwa mshahara wa milioni 11 na posho lukuki. Mbunge asiehudhuria vikao vya bunge asipewe mshahara na aondolewe ubunge.
Lazima tufike mahala tuchoke kulindana maana nchi inadidimia

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments