[wanabidii] Msitu na Nyika: Watanzania Wakimbilie Wapi Sasa?

Monday, November 04, 2013


Nyumba yako inaungua; unakimbilia kwa jirani nako kuna moto; mnapiga mayowe watu waje kuwasaidia kumbe na wao wanajitahidi kuokoa nyumba zao. Unapofuatilia kwa karibu unakuta kuwa moto umeweshwa na wenye nyumba wenyewe. Watu wanaunguza nyumba zao wenyewe kwa kukomoana na kule unakotaka kwenda kujihami nako wenye nyumba wamewasha moto; mtaa mzima watu wanalia 'moto moto'! Hakuna wa kuzima moto kwani nani atajitolea kuzima moto wakati anafikiri unaunguza chumba cha mwingine; japo nyumba ile ile?

Wanaacha chumba kimoja kimoja kinaungua wakiamini kuwa nyumba nzima haitateketea; au wanajitahidi kulinda vyumba vingine visishike moto lakini hawajitokezi kuzima moto kwenye chumba cha ndugu yao! Moto wayaka, moto wayaka!

Watanzania wanatafuta pa kukimbilia; dalili zinaonesha kuwa tutaamka siku moja na kujikuta tunakanyaga majivu. Tutaogopa hata kuulizana moto ulitoka wapi na kwanini hatukuuzima! Maskini Watanzania waliokuwa na matumaini kuwa labda wanaweza kupata mahali pa kuhifadhi utu wao wanajikuta taratibu wakishudia tumaini likitoweka taratibu kama wingu linalopeperushwa na upepo au kama umande unavyotoweka pale mwangaza wa jua unapobusu na kuikumbatia siku mpya!

Uchaguzi wa serikali za mitaa ni chini ya mwaka mmoja sasa; uchaguzi mkuu chini ya miaka miwili, Katiba Mpya ndio hata sijui tuseme vipi na hapo hatujagusa ile ya Tanganyika. Elimu ya nchi yetu inakwenda yoyomama, huku uchumi wetu ukizidi kuwekwa mikononi mwa wageni huku wenye nchi wakitukanwa hadharani bila kukasirishwa! Wakati mambo muhimu ya taifa yanahitaji kufuatiliwa wenye kuitwa viongozi wanajitahidi kushindana siasa za mipasho na demokrasia ya kejeli!

Watanzania wakimbilie wapi sasa; tumaini lao liende wapi; nani atasimama kuwaongoza kiukweli? Nani atawaongoza kuzima moto usio wa lazima au tusubiri tuone nyumba ya nani itabakia ndio tuikimbilie? Vipi kama kijiji kizima kitachomwa; watu wajiandae kwenda kijiji cha jirani?

http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/548250-msitu-na-nyika-watanzania-wakimbilie-wapi-sasa.html

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments