Mwandishi wa gazeti la Mwananchi Fredy Azzah ameandika habari inayobainisha madudu zaidi katika upangaji mpya wa alama na madaraja kama ambavyo ilitangazwa na serikali. Dondoo chache zinazojitokeza kwenye habari hiyo ni kwamba.
1. Kuna kamati iliundwa na wizara ya elimu kufanya uchunguzi na kuja na mapendekezo ya viwango vipya vya ufaulu na utaratibu wa CA. Kamati hiyo ilikabidhi ripoti yake wizarani Septemba mwaka huu; na mapendekezo yalikuwa kama ifuatavyo: A=80-100, B=70-79, C=50-59, D=40-49, E=35-39, F=0-34; Kamati ilipendekeza kuwa alama za CA (alama endelevu ya mwanafunzi shuleni) iwe 25.
2. Kwa mujibu wa kitabu kinachoonesha viwango vya ufaulu duniani kinachotolewa kila mwaka; International Qualification, baada ya Tanzania kutangaza alama mpya; sasa inakuwa nchi inayoongoza duniani kwa kuwa na alama za chini za ufaulu
3. Mwandishi alimhoji afisa mwandamizi wa Baraza la Mitihani (NECTA) kuhusu hizo alama za CA; afisa huyo alisema kuwa walimu wengi hutuma Baraza alama kuanzia 70 kati ya 100 za CA, zikionesha uwezo wa wanafunzi walio nao-watakaofanya mtihani mwaka huo; ambazo kati ya 40=mtoto anakuwa amepata alama 28 kabla ya mtihani wa mwisho; ambapo hiyo tayari ni E. Afisa huyo ametahadhalisha kuwa-hata mwanafunzi asipojibu chochote kwenye mtihani wa mwisho anaweza kuwa na E tayari kwenye somo hilo. Kwa kuzingatia hilo; Baraza wao walishauri kuwa alama ya CA, isizidi alama ya kufeli. Hivyo basi kama F mwisho ni 19; huenda alama zake na CA zingekuwa chini ya hapo=kama tahadhari ya Baraza ingezingatiwa.
4. Afisa huyo wa Baraza anasema Baraza walipoyapanga upya matokeo ya wanafunzi ya mwaka 2012 kwa kutumia alama na madaraja mapya; anasema ufaulu kwa Div 1 mpaka 4 ulipanda mpaka kufikia asilimia 93.74, ambapo wanafunzi asilimia 6.26 tu ndio wangefeli. Huo ni ufaulu mkubwa sana ukilinganisha na matokeo jinsi yalivyokuja wakati huo; Div 1 hadi 4 walifaulu asilimia 43.08. Hili ndilo swali tulilokuwa tunauliza wadau hata kwenye tamko letu. Iweje serikali itake kuona matokeo mazuri bila kuboresha ufundishaji na ujifunzaji ambao ndio ungepandisha matokeo?
Tafakari. Toa Maoni.
Unaweza kuisoma habari hiyo zaidi kwa kufungua hapa
http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-Madudu--yaibuliwa/-/1597296/2063298/-/edmu63/-/index.html
-- 1. Kuna kamati iliundwa na wizara ya elimu kufanya uchunguzi na kuja na mapendekezo ya viwango vipya vya ufaulu na utaratibu wa CA. Kamati hiyo ilikabidhi ripoti yake wizarani Septemba mwaka huu; na mapendekezo yalikuwa kama ifuatavyo: A=80-100, B=70-79, C=50-59, D=40-49, E=35-39, F=0-34; Kamati ilipendekeza kuwa alama za CA (alama endelevu ya mwanafunzi shuleni) iwe 25.
2. Kwa mujibu wa kitabu kinachoonesha viwango vya ufaulu duniani kinachotolewa kila mwaka; International Qualification, baada ya Tanzania kutangaza alama mpya; sasa inakuwa nchi inayoongoza duniani kwa kuwa na alama za chini za ufaulu
3. Mwandishi alimhoji afisa mwandamizi wa Baraza la Mitihani (NECTA) kuhusu hizo alama za CA; afisa huyo alisema kuwa walimu wengi hutuma Baraza alama kuanzia 70 kati ya 100 za CA, zikionesha uwezo wa wanafunzi walio nao-watakaofanya mtihani mwaka huo; ambazo kati ya 40=mtoto anakuwa amepata alama 28 kabla ya mtihani wa mwisho; ambapo hiyo tayari ni E. Afisa huyo ametahadhalisha kuwa-hata mwanafunzi asipojibu chochote kwenye mtihani wa mwisho anaweza kuwa na E tayari kwenye somo hilo. Kwa kuzingatia hilo; Baraza wao walishauri kuwa alama ya CA, isizidi alama ya kufeli. Hivyo basi kama F mwisho ni 19; huenda alama zake na CA zingekuwa chini ya hapo=kama tahadhari ya Baraza ingezingatiwa.
4. Afisa huyo wa Baraza anasema Baraza walipoyapanga upya matokeo ya wanafunzi ya mwaka 2012 kwa kutumia alama na madaraja mapya; anasema ufaulu kwa Div 1 mpaka 4 ulipanda mpaka kufikia asilimia 93.74, ambapo wanafunzi asilimia 6.26 tu ndio wangefeli. Huo ni ufaulu mkubwa sana ukilinganisha na matokeo jinsi yalivyokuja wakati huo; Div 1 hadi 4 walifaulu asilimia 43.08. Hili ndilo swali tulilokuwa tunauliza wadau hata kwenye tamko letu. Iweje serikali itake kuona matokeo mazuri bila kuboresha ufundishaji na ujifunzaji ambao ndio ungepandisha matokeo?
Tafakari. Toa Maoni.
Unaweza kuisoma habari hiyo zaidi kwa kufungua hapa
http://www.mwananchi.co.tz/
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments