[wanabidii] KUTESWA KWA DR ULIMBOKA NA MASLAHI YA NCHI

Tuesday, November 12, 2013

KUTESWA KWA DR ULIMBOKA NA MASLAHI YA NCHI

Ndugu zangu

Siku na miezi kadhaa imepita tangu kuteswa kwa Dr Steven Ulimboka ambaye alikuwa kiongozi wa chama cha madaktari na pia kiongozi wa mgomo wa madaktari ambao waliapa hutokuwa na kikomo cha mgomo huo .

Mgomo huu ulisababisha huduma nyingi za kimatibabu wa wagonjwa kuzorota haswa hospitali za serikali , watu wengi walipoteza maisha , ndugu zao , jamaa na marafiki wote hawa hawakuangaliwa lakini aliyegusa nyoyo za watu ni dr ulimboka kutokana na nafasi yake katika mgomo huu .

Tukumbuke viongozi wengi walioendesha mgomo huu walikuwa na kazi za ziada haswa katika hospitali binafsi kwahiyo mgomo ulipokuwa unaendelea kwenye hospitali za serikali wao waliendelea na huduma zao kupitia hospitali binafsi au sehemu nyingine ambazo hazikuwa na vikwazo kwao .

Vile vile wale wanafunzi waliokuwa wanafanya masomo kwa vitendo walisitishwa masomo kwa muda kutokana na mgomo huu , ilibidi wauguzi waliostaafu kurudi kazini na hata wengine kutoka jeshi la polisi na jeshi la wananchi Tanzania .

Hali ilikuwa mbaya kweli na jamii hii ilihitaji msaada toka kwa serikali waliyoiweka madarakani kwa njia ya kura miezi michache iliyopita tu , serikali iliangalia maslahi makubwa zaidi kwa jamii hiyo ili mzozo huu usiendelee na kuwa mbaya zaidi .

Wakati serikali ikichukuwa hatua hizi , serikali hiyo hiyo ilikuwa iko kwenye mikakati ya kuboresha huduma za afya nchini kwa vifaa , kusomesha wanafunzi zaidi ndani na nje ya nchi pamoja na kujenga majengo mapya na kukarabati ya zamani .

Natoa pole kwa wale walioathirika na mzozo huu akiwemo dr steven ulimboka aliyekuwa kiongozi wa mgomo huu na aliyetakiwa kuwa mfano bora wa kuongoza wenzake katika meza ya mazungumzo ili kutatua mzozo huu kwa njia ya amani lakini haikuwa hivyo mpaka pale nguvu za ziada zilipotumika kulazimisha hivyo .

Muhimu ni kujua maslahi ya umma ni zaidi ya mtu mmoja mmoja na serikali ina uwezo wa kuhakikisha maslahi ya umma yanapatikana itakapohitajika .

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments