Ngoma Africa Band aka FFU Kutumbuiza mjini Bremen,Ujerumani
Usiku Jumamosi 20.Nov.2013
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa band" a.k.a FFU watarajiwa kutumbuiza usiku wa jumamosi 23.November 2013 katika ukumbi wa Übersee-Museum mjini Bremen,mchini Ujerumani.
Wakazi wa jiji la Bremen na miji ya jirani watapata burani ya kung'oa na sululu
kutoka kwa mzimu wa muziki Ngoma Africa band ambayo maarufu sana kwa kuwatia kiwewe washabiki wake kila wapandapo jukwaani.
Onyesho hilo limeandaliwa na makumbusho ya Oversee Museum ya jiji la Bremen kwa kushirikiana na Pan African Organization.
Ngoma Africa band wataanza kutumbuiza majira ya saa. 4.00 usiku na kabla ya hapo kutakuwa na maonyesho mbali mbali ya bidhaa za kiafrika,pamoja na vyakula.
Bendi ya "Ngoma Africa " ambayo inadumu kwa muda wa miaka 20 imetajwa kuwa ndio bendi ya mwanzo ya kiafrika kufanikiwa kudumu katika medani ya muziki na kujizolea mamilioni ya washabiki katika kila kona duniani.
Watafiti wa mambo ya muziki wameitaja bendi hiyo kuwa inatumia kila nafasi
waliyo nayo kuwanasa washabiki wake,na imetajwa mara nyingi kuwa ni bendi bora na kuchukuwa TUZO za kimataifa, ni bendi ambayo imepachikwa majina mengi mengi ya utani na kiusanii kama a.k.a "FFU Ughaibuni" ,aka "Watoto wa mbwa" chini ya uongozi wake Kamanda Ras Makunja wa FFF, Mtawala wa
himaya ya " Anunnaki Empire "
Usikose kuwasikiliza at
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments