On Friday, November 15, 2013 2:21 PM, Laurance Rukundo <rukundo88@yahoo.com> wrote:
Je umefika wakati wa viongozi kuapa huku wameshika Katiba ya nchi?
Naandika hivi, baada ya kuaangalia na kutafakari kwa makini sana kuhusu hii hali ya viongozi wetu kuapa huku wameshikilia Vitabu vya Dini na baadaye hufanya kinyume na yakiyomo katika vitabu hivyo vitakatifu.
Kwani naamini ndani ya nasfi yangu kuwa 99.9% ya viongozi hawajui kwa undani nini Vitabu hivi Vitakatifu vinasema, nk katika mambo kufanya mambo mema.
Hii imenifanya kuhisi ya kuwa hawa viongozi kwakuwa wanaamini wakitenda dhabi watasamehewa kaka Vitabu vinavyo sema/ vilivyo andikwa, labda ndiyo maana wakisha apa kwa kutumia vitabu hivyo Vitakatifu huachia hapo waliyo yasema wakati wanaapa na kufanya mengine wakishakalia kiti cha uongozi au kuingia madarakani.
Naona ni vyema kabla kugombania uongozi wanchi wahojiwe kama wana aielewe katiba ya nchi inataka nini kitekelezwe, ili kiongozi huyo anapo apa kwa kushikilia Katiba anajua anacho sema na naikitokea kavunja moja ya sheria iliyomo ndani ya katiba,itakuwa rahisi kumtia hatiani bila kupingwa.
Ikiwa tumebadirika kimawazo,kwanini tusibadishemfumo wa kuapa kwa kutumia Vitabu vya Dini
0 Comments