[wanabidii] BARUA YA WAZI KWA MWENYEKITI WA CHADEMA FREEMAN MBOWE

Wednesday, November 06, 2013
Ujumbe wangu Kwa Mheshimiwa sana na Rafiki yangu Freeman Alikaeli Mbowe Mwenyekiti wa sasa wa Chadema.

Siasa ni utashi wa akili Kubwa.Ukiwa Mwanasiasa Lazima ujitambue kuwa na akili kubwa.Lakini usipojitambua utakuwa unakaribisha kutumbukia shimoni wa
kati wa Vita.Vita ya Siasa upigwana kwa sababu ya Masilahi ya Uchaguzi na Masilahi ya Kimsimamo katika kushinda Maamuzi ya kuungwa mkono Hoja yako.

Vita ya Siasa anayopigana Leo Mbowe ndani na nje ya chama chake ni Vita ya kueendelea kuaminiwa kuwa Mwenyekiti na wajumbe wa mkutano mkuu wa Chadema kwa kupigiwa kura.Vita hii siyo Rahisi kama wasiowanasiasa na wachambuzi wanavyoweza kuitazama ni vita ya akili kubwa kwa kushirikisha organ zote za Ubongo.Inatakiwa kupiganwa kwa akili zenye utashi wa Busara na Hekima bila kudhuru chama na wapiga kura.Maana mkitanguliza ile dhana ya lazima nishinde nikiwa hai au nimekufa ,utajikuta unakuwa Mwenyekiti lakini huna chama sasa utaongoza nini,iwapo unapata unachokitaka lakini umeua misingi utasimamaje!

Nakushauri cheza vita hii kwa akili,Usitumie zile akili za kuwa -eliminate wagombea wenza kama ilivyowahi kutokea uko Nyuma mlivyompoteza Kamanda na Mwanamara mwenzangu Zakayo Chacha Wangwe ,Siyo kwa njia hiyo tu hata ile ya kutaka kuwachinjia Bahariani wagombea wenzako kwa kutotaka mshindane katika Sanduku la Kura ,kwa kutumia Kigezo Cha Uenyekiti wako na Katibu Mkuu kukata Majina ya waomba uongozi kama wewe.Utakuwa umefanya kosa kubwa na utakuwa umeruhusu kuongozwa na akili ndogo na za kitoto.Na vita itakushinda iwapo wapiga kura wataamua kutumia akili zao kukijenga chama lazima watakudondosha ili kunusuru Chama chao.Hivyo nakusihi Tumia utashi wako na Hekima uliyoivuna wakati wa uongozi wako kusema sasa basi UCHAGUZI NI KWA KILA MWENYE SIFA NA NI HURU NA HAKI YA KILA MWANACHAMA,Hakika ukifanya hivyo utafauru.

Kuacha malumbano ya wapambe wako yakomae kwenye vyombo vya habari dhidi ya wale wasiokuunga mkono ni kukisambaratisha chama hiki nadhimu cha upinzani nchini na kufanya Watanzania wenye mapenzi mema nacho kuhoji ni kwa nini haya yanatokea na uko kimya?Unafaidikaje na Hii migogoro ya ndani ya chama unachokiongoza? Na kama kiongozi kwa nini umeshindwa kuimaliza? Je unategemea upewe uongozi ili ufanye nini kama unashindwa kusimamia mambo madogo kama hayo? Migogoro midogo kabisa kama ya Zitto Z Kabwe na Lema leo ukiwa huna serikali Je ukipewa serikali utaweza huku kutatua migogoro,ukienda huku dawa hakuna Hospitali ukienda huku,Maji safi na salama hakuna,mara mafuriko na maafa sehemu fulani ya nchi,Mara wabunge wanataka nyongeza ya posho,mara wafanyakazi nyongeza ya mishahara kila mahari migogoro utaweza kukisimamia chama wakati huo kiisimamie serikali yako ya Daktari Slaa kama watanzania kuna siku wataamua kuwapa nchi waonje matunda mema ya nchi mnayowahibiria kila siku! Au wataonja shubiri kuliko mliyokuwa mkiidai kutokana na udhaifu wako wa uongozi.

Kabla ujaingia kwenye uchaguzi huu kubali kukiweka chama chako sawa,Usije ukahukumiwa na kura za hasira.Maana utawafukuza wangapi na kuwavua uanachama wangapi? Utamsemea nani na nani mabaya na kupika Fitna kabla hujadhihirika? Utaaua wangapi? Moto wa Mabadiliko hauzimishwa kwa Maji baridi,Sio ninyi huwa mnaiambia CCM haiwezi kuzima mapinduzi ya Fikra kwa kutumia dola? Sasa wewe huoni unavyozima mapinduzi ya Fikra kwa Kutumia Rungu la Katibu Mkuu na Wewe mwennyewe kama Mwenyekiti?Angalia hasira za wapiga kura zisikuangukie.

Hebu kaka yangu jiulize ni kwa nini Hoja zenu sikuhizi mawaziri vivuli wakiisha wasilisha zinakuwa hazina contribution ya maana kutoka kambi yako unayoiongoza kama kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni nafasi uliyopewa kwa Heshima ya KUwa mwenyekiti wa Chama kikuu cha Upinzani Bungeni.Nafasi hii kumbuka ilivyotendewa kazi na Hamad Rashid leo unaweza kujipima katika viatu vya Hamad Rashid kweli huoni kupwaya! Umeusambaratisha umoja wa wabunge wako mwenyewe hebu Rejea zile Busara na Hekima zako nilizokutambua unazo wakati wote.Uchaguzi huu usikupofushe Macho .Weka VIFANGA WAKO UNAOWALEA PAMOJA.Ili kukijenga Chama ninachoamini umetumia Muda na Mali zenu nyingi kukijenga.Kila la KHERI.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments