Habari yako mheshimiwa Rais?
Kwanza kabisa heshima yako, shikamoo na Pole sana na kazi za kulitumikia Taifa letu. Mimi ni mwalimu wa shule ya msingi Matakapola, iliyopo Ilala hapa Dar. Haina haja ya utambulisho sana, naomba niende kwenye dhumuni la hii barua.(Ila ombi, naomba hii barua uisome wewe mwenyewe Rais, kama kuna servant anakusomeaga, aishie hapa. Aiweke store siku ukiwa na muda wa ziada wewe ndio uisome taratibu. Tafadhali sana. Ijumaa iliyopita mshahara wangu uliingia kwenye account yangu. Asante sana ingawa ni jasho langu. Basi yafuatayo ni matumizi yangu tokea Ijumaa hadi leo:
1. Kodi ya chumba (miezi 3)- Tsh 60,000, bili ya maji mwezi huu Tsh. 4,000 na ya
umeme Tsh.5,000
2. Chakula cha akiba kwa huu mwezi (Unga 10kg, Mchele 10kg, Maharage 5kg, Mafuta 2Lts)-Tsh 42,000.
3. Mazaga zaga (Mazagazaga ni vitu vidogo vidogo ila vya muhimu sana) ya jikoni
kama majani ya chai, chumvi, mkaa, kiberiti, mafuta ya taa-Tsh.10,000
4. Mwalimu usafi, imebidi nipitie mitumbani (huku ni sehemu unakoweza pata
kitu cha bei kubwa kwa bei nafuu) nipate nguo za kubadilisha, maana hizi
wanafunzi wamenizoea nazo. Hapa nili spend kama Tsh.15,000 na nikazipeleka
kwa fundi kuzirekebisha (Efect (Madhara) mojawapo ya nguo za mitumbani ni
kawaida kuwa oversize, ombea isiwe undersize, na ukishanunua hakuna guarantee wala kurudisha) hapa nikatumia tena Tsh 5,000. Pia nikaenda duka la vipodozi kudaka body spray (Tsh.5,000), Mafuta ya BabyCare (Tsh.1000).
5. Wazazi wangu wameteseka sana kunisomesha, hivyo fadhila muhimu kuwarudishia kwa hiki hiki kidogo nipatacho. Nika wa M-Pesa Tsh.40,000 ili watumie kubadilisha mboga juma pili na nusu iwasaidie kumalizia ada ya mdogo wangu Riziki, yupo ile shule uliyokuja izindua mwaka 2011/May/13 kijijini kwetu Mwankosi Mbozi Mbeya (au basi, sidhani kama unakumbuka, maana ulituahidi visima, barabara, madawati shuleni na kujenga bweni la wasichana, ila hadi leo umetuachia manyoya. Umekumbuka? Siku ile Ulivaa tai nyekundu, suti nyeusi na shati la drafti drafti jeupe. Na ulikuja na mama, yeye alivaa full vitenge vya chama! umeKumbuka?)
6. Kuna hela ya nauli kwenda na kurudi kila siku shuleni (Tsh.600 per day), vitafunwa asubuhi kila siku (Tsh.200 per day), na vitu visivyo nunulika kwa wingi, maana vitaharibika kama vitunguu, sabuni, nyanya, nazi,karoti, etc nakadiria Tsh.10,000 kwa mwezi.
7. Mheshimiwa kuna vitu havizuiliki kama vocha, nyama wakija wageni, kwenda hospitali, bado kutoka out mara moja moja (Yaani kama wewe unavoendaga Sydney kula mbuzi, na sisi tunaenda kwa mama Lucy sinza, kula vifaranga).
8. Kuna Hiyo pesa tunaiita hela ya emergence kama michago ya mtaani, sadaka,
misiba, kiatu/nguo kwa fundi...etc Mheshimiwa kama ulisoma vizuri hesabu kama mimi, roughly hapo ni jumla kama Tsh.210,000 nikiongeza na pesa ya hitaji no.7&8 jumla kama Tsh.250,000. Mheshimiwa kutaja mshahara wangu hapa si vizuri, lakini kwakuwa mama hapo nyumbani ameshawahi kuwa mwalimu naomba nikusumbue, hebu muulize walimu grade A, tunaoanza kazi tunalipwaje? Kumbuka hapa bado niko
peke yangu (Single Boy), sina hata mpenzi. Hivi nina ndoto za kuoa kweli ukitizama iko kipato? Nikiwa na mtoto je? Akianza kusoma je? Nawaza sijui nikakope NMB au FINCA au VICOBA sijui Bay Port au SACCoS? Yaani sijielewi. Sikushawishi uniongeze mshahara, ninachoomba tu, fananisha kazi yangu na hiyo wanayofanya wabunge
"wako" niliowachagua, au hata kazi unayofanya wewe.Ndiyo. Wewe Mheshimiwa. Kuna watu wananishauri nianzishe tuition, lakini mimi ni mzalendo wa pili baada ya Nyerere, itakuwaje watoto wa maskini? Wasisome? Hapana, this is not fair (Sijui kama
umeshawahi waza hili Mh.) Wengine wamesema nianzishe biashara. Sijui hata pa kupata mtaji, pili sio vizuri maana nitaelekeza nguvu nyingi kwenye biashara kuliko kazi ya kuelimisha hili Taifa, narudia mimi ni Mzalendo. Hawa waliosema niache kazi wapotezee (achana nao). Ok Mh, naomba nisiongee sana maana una kazi, safari
na mambo mengi sana. Nisikuchoshe. Natumaini ombi langu (Kama umesahau la
kuweka hapo matumizi yako ya mshahara) litasikilizwa na kufanyiwa kazi. Wako katika kujenga, kuelimisha na kuandaa Taifa lijalo
Mwl.
-- Kwanza kabisa heshima yako, shikamoo na Pole sana na kazi za kulitumikia Taifa letu. Mimi ni mwalimu wa shule ya msingi Matakapola, iliyopo Ilala hapa Dar. Haina haja ya utambulisho sana, naomba niende kwenye dhumuni la hii barua.(Ila ombi, naomba hii barua uisome wewe mwenyewe Rais, kama kuna servant anakusomeaga, aishie hapa. Aiweke store siku ukiwa na muda wa ziada wewe ndio uisome taratibu. Tafadhali sana. Ijumaa iliyopita mshahara wangu uliingia kwenye account yangu. Asante sana ingawa ni jasho langu. Basi yafuatayo ni matumizi yangu tokea Ijumaa hadi leo:
1. Kodi ya chumba (miezi 3)- Tsh 60,000, bili ya maji mwezi huu Tsh. 4,000 na ya
umeme Tsh.5,000
2. Chakula cha akiba kwa huu mwezi (Unga 10kg, Mchele 10kg, Maharage 5kg, Mafuta 2Lts)-Tsh 42,000.
3. Mazaga zaga (Mazagazaga ni vitu vidogo vidogo ila vya muhimu sana) ya jikoni
kama majani ya chai, chumvi, mkaa, kiberiti, mafuta ya taa-Tsh.10,000
4. Mwalimu usafi, imebidi nipitie mitumbani (huku ni sehemu unakoweza pata
kitu cha bei kubwa kwa bei nafuu) nipate nguo za kubadilisha, maana hizi
wanafunzi wamenizoea nazo. Hapa nili spend kama Tsh.15,000 na nikazipeleka
kwa fundi kuzirekebisha (Efect (Madhara) mojawapo ya nguo za mitumbani ni
kawaida kuwa oversize, ombea isiwe undersize, na ukishanunua hakuna guarantee wala kurudisha) hapa nikatumia tena Tsh 5,000. Pia nikaenda duka la vipodozi kudaka body spray (Tsh.5,000), Mafuta ya BabyCare (Tsh.1000).
5. Wazazi wangu wameteseka sana kunisomesha, hivyo fadhila muhimu kuwarudishia kwa hiki hiki kidogo nipatacho. Nika wa M-Pesa Tsh.40,000 ili watumie kubadilisha mboga juma pili na nusu iwasaidie kumalizia ada ya mdogo wangu Riziki, yupo ile shule uliyokuja izindua mwaka 2011/May/13 kijijini kwetu Mwankosi Mbozi Mbeya (au basi, sidhani kama unakumbuka, maana ulituahidi visima, barabara, madawati shuleni na kujenga bweni la wasichana, ila hadi leo umetuachia manyoya. Umekumbuka? Siku ile Ulivaa tai nyekundu, suti nyeusi na shati la drafti drafti jeupe. Na ulikuja na mama, yeye alivaa full vitenge vya chama! umeKumbuka?)
6. Kuna hela ya nauli kwenda na kurudi kila siku shuleni (Tsh.600 per day), vitafunwa asubuhi kila siku (Tsh.200 per day), na vitu visivyo nunulika kwa wingi, maana vitaharibika kama vitunguu, sabuni, nyanya, nazi,karoti, etc nakadiria Tsh.10,000 kwa mwezi.
7. Mheshimiwa kuna vitu havizuiliki kama vocha, nyama wakija wageni, kwenda hospitali, bado kutoka out mara moja moja (Yaani kama wewe unavoendaga Sydney kula mbuzi, na sisi tunaenda kwa mama Lucy sinza, kula vifaranga).
8. Kuna Hiyo pesa tunaiita hela ya emergence kama michago ya mtaani, sadaka,
misiba, kiatu/nguo kwa fundi...etc Mheshimiwa kama ulisoma vizuri hesabu kama mimi, roughly hapo ni jumla kama Tsh.210,000 nikiongeza na pesa ya hitaji no.7&8 jumla kama Tsh.250,000. Mheshimiwa kutaja mshahara wangu hapa si vizuri, lakini kwakuwa mama hapo nyumbani ameshawahi kuwa mwalimu naomba nikusumbue, hebu muulize walimu grade A, tunaoanza kazi tunalipwaje? Kumbuka hapa bado niko
peke yangu (Single Boy), sina hata mpenzi. Hivi nina ndoto za kuoa kweli ukitizama iko kipato? Nikiwa na mtoto je? Akianza kusoma je? Nawaza sijui nikakope NMB au FINCA au VICOBA sijui Bay Port au SACCoS? Yaani sijielewi. Sikushawishi uniongeze mshahara, ninachoomba tu, fananisha kazi yangu na hiyo wanayofanya wabunge
"wako" niliowachagua, au hata kazi unayofanya wewe.Ndiyo. Wewe Mheshimiwa. Kuna watu wananishauri nianzishe tuition, lakini mimi ni mzalendo wa pili baada ya Nyerere, itakuwaje watoto wa maskini? Wasisome? Hapana, this is not fair (Sijui kama
umeshawahi waza hili Mh.) Wengine wamesema nianzishe biashara. Sijui hata pa kupata mtaji, pili sio vizuri maana nitaelekeza nguvu nyingi kwenye biashara kuliko kazi ya kuelimisha hili Taifa, narudia mimi ni Mzalendo. Hawa waliosema niache kazi wapotezee (achana nao). Ok Mh, naomba nisiongee sana maana una kazi, safari
na mambo mengi sana. Nisikuchoshe. Natumaini ombi langu (Kama umesahau la
kuweka hapo matumizi yako ya mshahara) litasikilizwa na kufanyiwa kazi. Wako katika kujenga, kuelimisha na kuandaa Taifa lijalo
Mwl.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments