Leo wanafunzi wa kidato cha nne wameanza mitihani yao ya Taifa. Tunawaombea wawe watulivu na makini katika kipindi chote cha mitihani-na wafanye vizuri, inshaallah! Baadhi yao watakuwa wamevurugwa na taarifa za kupangwa upya alama na madaraja-hata hivyo tunawasihi wasome kwa bidii na kuucha mjadala huu uendelezwe na wadau wengine. Wapande vizuri, ili wavune vizuri! Wapo ambao wanashangilia kuwa sasa mambo yamekuwa 'mswano' kuwa basi hawatafeli tena kutokana na taarifa za upangaji upya wa alama na madaraja. Huenda hilo likabadilika kwa nguvu ya umma-na baadaye wakahesabiwa wamefeli. Hata hivyo, kilicho muhimu kwao ni kile kilichopo na kitakachoendelea kuwepo vichwani mwao sasa na baada ya kumalizq masomo yao; yaani maarifa, ujuzi, ubunifu, kujiamini, ari ya kufanya kazi, uzalendo, n.k. ELIMU NI UWEZO SIO CHETI!
-- Source : Haki Elimu
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments