Tangu mchezo wa Tuition kwa wanafunzi uanze hapa Tanzania, wanafunzi wamekuwa wavivu na kutowajibika tena. Nilipokuwa secondary miaka ya 80 na 90 nilifundishwa ili kufaulu jitihada za mwanafunzi mwenyewe ni 60% na 40% ni mwalimu pamoja na vitabu.
Cha kusikitisha ni kwamba siku hizi wanafunzi hawana nafasi tena ya kujisomea wenyewe. Kila wakati mwalimu yupo mbele yao. 80% ya muda wa mwanafunzi mwalimu yuko mbele yake. SPOON FEEDING. Mwalimu akitoka mbele yake, mwanafunzi hawezi kujishughulisha kwa kurudia alichofundishwa au kutafuta kwenye vitabu (library) ili kujipanua kwa alichosikia darasani. Hajui afanye nini.
Akitoka shuleni saa 9 mchana, saa kumi anamkuta mwalimu mwingine nyumbani hadi saa 2 au 3 usiku. Mwanafunzi hana muda wa KUCHEUA alichofundishwa. Hata home work hana muda nazo.
Mbaya zaidi, mzazi na mwanafunzi wote wanaamini kuwa pasipo TUITION, mtoto anafikiri hawezi faulu na mzazi pia anaamini mwanangu hawezi faulu.
Kwa kifupi TUITION IMEUA UWEZO WA WANAFUNZI KUFIKIRI.
Tuition jamani ifutwe. Kwanza waalimu wanatumia njia hiyo kwa kutowajibika vema muda wa shule maana anajua kuwa kuna cha juu baadae.
0 Comments