[wanabidii] MWANAMKE APIGWA RISASI KATIKA OFISI ZA TRA ARUSHA

Wednesday, October 30, 2013
Mwanamke mmoja amepigwa risasi ya mkononi kutokana na uzembe wake mwenyewe.

Mwanamke huyo alifika maeneo ya TRA ambako kuna tawi la CRDB - Mapato eneo lisiloruhusiwa. Askari walimuelekeza eneo hilo haliruhusi lakini alikataa na kuingia ndani ya bank kwa ajili ya shughuli za bank anazozijua yeye.

Askari hao walimfuata tena ndani na kumwambia akatoe gari lakini mwanamke huyo kwa nyodo alimjibu askari huyo aachane nae.

Kuona hivyo askari walikwenda kutoa upepo kwenye matairi ya gari yake ili kama alikuwa na watu wengine wenye nia mbaya wahindwe kutekeleza mpango wao.

Yule mwanamke aliporudi na kukuta gari yake imetokewa upepo alikwenda moja kwa moja kwenye gari na kutoa bastola kisha akaenda kwa walinzi walipo huku akiwatisha atawaua. Katika hali ya taharuki yule mwanamke akakoki bunduki kwa lengo la kuitumia na ndipo askari akipomuhai risasi ya mkononi.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio mwanamke huyo hajulikani alipata wapi ujasiri wa aliyoyafanya.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments