[wanabidii] MAKAMPUNI YA SIMU YANATUIBIA

Friday, October 11, 2013
Ndugu watanzania wenzangu tuzinduke haya makampuni ya simu yanatuibia. Wanajifanya wanatoa offer eti sh 600 unapewa dakika kama 20 hivi za kupiga simu . Lakini cha ajabu wanakupa masaa 24 uwe umeshatumia hizo dk zao walizokupa vinginevyo muda huu ukiisha kama hajatumia dk zako zote umeliwa. Huo ni wizi mtupu wangekuwa waungwana wangetupa hizo dakika bila kutuwekea muda wa kuzitumia mtu awe huru kuzitumia anapozihitaji. Lakini wanalazimisha watu kupiga simu hata zisizo za lazima ili tuu mtu amalize dakika alizopewa kabla muda haujaisha.
Naomba haya makampuni pamoja na hizo promotion zao wasitoe muda ila watoe dakika ili mtu awe huru kuzitumia muda autakao mpaka ziishe.

Share this :

Related Posts

0 Comments