AMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA
Kutokana na marekebisho hayo, utaratibu wa kutoa Leseni za Biashara BILA MALIPO uliondolewa na kusitishwa na Serikali tarehe 30 Juni, 2013. Leseni za Biashara zilizotolewa kuanzia tarehe 1 Julai, 2004 hadi 30 Juni, 2013 ambazo hazikuwa na UKOMO zinatakiwa kupelekwa kwenye Mamlaka zilizotoa Leseni hizo, ili zihuishwe na kulipiwa ada kwa madhumuni ya kuongeza mapato kwa Serikali.
Kila mfanyabishara mwenye Leseni ya Biashara anapaswa kujaza Fomu ya Maombi ya Leseni ya Biashara na kuambatisha Leseni ya Biashara aliyonayo na kuiwasilisha katika Mamlaka husika, kwa ajili ya kuhuisha na kulipia ada. Maombi yapelekwe katika Mamlaka iliyotoa Leseni husika. Kwa Leseni za Biashara za kundi "A" kama ilivyoainishwa kwenye Fomu ya Maombi ya
Leseni ya Biashara TFN Na. 211ya 2004 hutolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara. Maombi hayo yawasilishwe katika Ofisi za Wizara ya Viwanda na Biashara zilizopo Barabara ya Sokoine Jengo la NSSF-"Water front", Ghorofa ya Nne chumba Na. 416. Kwa wale Wafanyabiashara wa Kundi "B" kama ilivyoainishwa kwenye Fomu ya Maombi ya Leseni ya Biashara TFN Na. 211ya 2004 wafike Ofisi za Halmashauri za Majiji, Manispaa na Wilaya zilizo katika maeneo yao, watapata huduma kutoka kwa Maafisa Biashara wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Waombaji wapya wa Leseni za Biashara mnapaswa kujaza fomu ya maombi ya Leseni za Biashara na kuambatisha nyaraka kama inavyojieleza katika fomu ya maombi na kufuata hatua ya 1 hadi 5 kama ilivyoelezwa hapo juu.
Mnashauriwa kuhuisha na kulipia ada Leseni za Biashara mapema kabla ya tarehe 31 Desemba, 2013 ambapo adhabu na faini kwa wafanyabiashra watakaochelewa kuhuisha (Renew) itaanza kutolewa tarehe 1 Januari, 2014.
Wafanyabiashara mnatadharishwa kuwa hapa mjini kuna mawakala wasio waaminifu maarufu kwa jina la VISHOKA. Mnashauriwa kuwaepuka na muweke utaratibu wa kufuatilia Leseni za Biashara zenu wenyewe.
Kwa wale ambao, wameshaletewa Leseni za Biashara na mawakala waliowatuma mnashauriwa kwenda kwenye Mamlaka iliyotoa Leseni husika kwa ajili ya kufanya uhakiki kwa kuwa imebainika kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara wanaofanya biashara kwa kutumia Leseni batili (Feki)
TAFADHALI FIKA NA KUFANYA UHAKIKI KWA FAIDA YA BIASHARA YAKO.
MAELEZO ZAIDI YANAWEZA KUPATIKANA PIA KWA KUTUMIA ANUANI IFUATAYO:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Viwanda na Biashara,
S. L. P. 9503,
Simu Na-+255-22-2127897/8,
Fax: +255-22-2125832
Website – www.psmit.go.tz
DAR ES SALAAM.

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments