Nikiwa kama mtanzania niliye na uzalengo na mapenzi mema ya nchi yangu, na bila ushabiki wa kichama/kisiasa unaotawala maamuzi mengi katika nchi yetu; naomba kushauri yafuatayo katika kilichoendelea Bungeni na kinachoendelea nje ya bunge kuhusu upatikanaji wa Katiba mpya.
Na kama kuna mtu ana access na wabunge hasa walio wengi kimakundi kule bungeni, awashauri kuwa makini juu ya wanachokisema na kukishabikia bungeni na nje ya bunge kuhusu mchatakato wa katiba. Katika hoja hii ya kutafuta katiba mpya huenda personalities na sifa walizonazo kisiasa zisihusike sana na ikawalazimu kubadili mtazamo wao. Waheshimiwa hawa washauriwe kama yafuatayo. Kuna mahali inafika lazima nafasi na uwezo wa uongozi uwe mkubwa kuliko ideologies na ushabiki wa kisiasa au kichama...na katika mchakato wa kupata katiba mpya hatuna namna nje ya kuelezea umuhimu huo. Washauriwe yafuatayo:-
Kwanza wasaidiwe kuelewa au kukumbushwa maana ya katiba ya nchi...wajue kuwa ile sio katiba ya chama wala kikundi cha watu...sio katiba inayoamua leo na kesho tu bali inaamua mambo mengi ya sasa, ya siku za karibuni, ya muda mrefu, na ya vizazi vingi vijavyo. Kutunga katiba hakuhitaji kupoteza muda mwingi kwa kupongezana na kushabikiana. Kunahitaji kutulia kufikiri, kushawishi na kujadiliana. Kunahitaji kuwasikiliza sana wanaoona wanaonewa. Hata kama hawatapewa wanachotaka lakini waridhishwe kwa kushawishiwa kuwa ni kwa nini hawawezi kupata watakacho.
Katika hili, wajitahidi kuachana kasumba ya nani kaongea bali waangalie nini kimeongewa.
Wasitumie muda mwingi kumuangalia, kumchambua na kumkosoa mtoa maoni bali wafanye hivyo kuchambua

nini kimeongewa. Katika jambo hili, ukomavu wa kisiasa ni kutumia muda mwingi kwenye hoja badala ya kwa mtoa hoja.
Pili, wabunge (hasa walio wengi kimakundi) wajue kuwa hakuna katiba itatungwa bila ushirika wa jamii nzima na makundi yaliyomo na ikafanikiwa. Ni muhim sana kutafuta maridhiano (consensus) kwa nguvu zote. Kama CDM, Wazanzibari, CUF au kundi linguine lolote lile linanung'unika, linasusa au linalalamika; dawa sio kuwapuuza, kuwafukuza bungeni, wala kuwaita majina mabaya....hapana. Katika hili la katiba kufanya hivyo itakua kosa kubwa sana. Haitakiwi kwenda hivyo. Hawa wakiachwa pembeni na malalamiko yao bila kuridhishwa kwa hoja ni hatari sana kwa baadaye. Na kuridhishwa sio lazima kupata utakacho bali ni kupata maelezo sahihi yenye kuleta kuafikiana.
Tatu, wabunge wa CCM na serikali ioneshe ukomavu wake wa kisiasa na uzoefu katika kuongoza snchi kwa miaka mingi katika huu mchakato wa katiba. Badala ya kuwapuuza wenye malalamiko na wapinzani wao kisiasa, na kushindana nao kwa nguvu ya kitaasisi au kura; watumie uzoefu wao kujenga hoja zenye nguvu ya ushawishi. Watumie kila njia njema yoyote inayowezekana kuwafanya wenye malalamiko wajione wana sababu ya kushiriki, kuhusika na kuendelea na majadiliano.
Waone nao wanahusika na wana mchango muhim. Katika kikao kilichomalizika jana, kuna wakati AG aliongea na kwa sehemu alikua anajaribu kushawishi na katumia busara sana ikiwa ni pamoja na kutaja majina ya wapinzani (Lissu na Mdee) waliotoa michango yenye nguvu kwenye kamati.
Nakutazama kuongea kwa namna ile kma lugha sahihi ya kutafuta muafaka kwa ushawishi wa majadiliano.
Nne, wabunge walio wengi wakumbuke kuwa maslahi (interests) yao ya kisiasa ya leo hayawezi kuwa hayohayo siku zote. Yatabadilika kulingana na nani au chama gani kinaongoza; hali za kisiasa itakazojitokeza, uchumi na mengine. Hata kama chama kinatawa kitaendelea kuongoza, bado wanaweza kujikuta interest zao za kisiasa zinabadilika kutokana na mabadiliko ya sera, uongozi, na mambo mengine. Hivyo lazima waangalie mbali sana zaidi ya viti wanavyokalia leo na faida wanayoipata sasa. Wajue hiki wanachokishabikia leo nao kesho chaweza kuwa cha kulalamikiwa. Waangalie mbele sana...mbele kabisa ya siku za uhai wao kwa ajili ya watoto wao na vizazi vijavyo.
Tano, Wabunge washariwe kuwa, kwenye hili waende taratibu...wacheze kulingana na mdundo wa ngoma. Wakikimbilia kupitisha sheria zinazoamua aina ya katiba itakayopatikana, na kisha wakaharakisha kuhakikisha wana kitabu kipya chenye maandishi ya kisheria kinachoitwa katiba, mwisho wa siku itaitwa katiba ya watu fulani. Katiba itakosa legitimacy and acceptance ya umma...kuna watakaoona sio yao na italeta shida kubwa. Hivyo basi wajitahidi kutumia hoja zenye nguvu ya ushawishi kutafuta consensus.
Sita, Tusiwe na kauli za hawa/ hao/wao na sisi kwenye mjadala huu. Tuachane na mazoea ya mashindano ya kisiasa ambayo tumekua nayo kila wakati. Tujitahidi kujadiliana katika hili la katiba kama SISI na kwa ajili YETU. Waachane jazba, kejeli, mipasho na mengine yasiyojenga katika hili. Msikilizeni mjinga; msikilizeni ambaye hajasoma; msikilizeni ambaye kwa kawaida huwa anadharauliwa; msikilizeni muliyezoea kumdharau; msikilizeni kila mwenye hoja bila kujali uzito wake na mwisho tutafute consensus ya nini chawezekana na kipi hakiwezekani katika hoja husika.
Saba, wabunge (hasa walio wengi kimakundi) wawe makini ni dhana ya ubinafsi. Mwanadamu ni mbinafsi kwa hasili yake na mara nyingine hutumia ubinafsi huo hata kujiumiza mwenyewe.
Wasichangie hoja na kutoa maamuzi yenye ubinafsi uliopindukia. Wakumbuke mafundishoa ya MTENDEE JIRANI YAKO KAMA AMBAVYO UNGEPENDA WEWE KUTENDEWA. Zaidi sana kwa wao, wala huyu mtanzania wanayepingana naye sio jirani, ni mwenzao, ni sehemu yao na kwa jili yao wenyewe. Wote twaitaka Tanzania iliyo bora. Hakuna anayekataa hoja za katiba hii kwa madai ya kutaka katiba nzuri ya Rwanda au Burundi au Somalia. Wote wana mawazo mazuri ya kuijenga Tanzania tunayoitamani. Hivyo ni lazima kutafuta namana nzuri ya kuunganisha haya mawazo mazuri ya kila upande bila kudharauliana, kutukanana, kukashifiana na kuumizana.
Nane, wabunge waisaidie serikali na nchi yetu kupunguza gharama kubwa zisizo za lazima au zinazoweza kuokolewa. Wafanye kitu ambacho hakitalazimisha kurudiwarudiwa kwa sababu tu kila wanapokaa hawafanyi wakamaliza au wanafanya bila kuangalia makosa ya wazi ambayo ni lazima kurekebishwa ili kusonga mbele. Wakumbuke ni gharama kubwa sana tangu kuandaa mswada hadi kuupeleka bungeni na kuupitisha. Wajue ni gharama kubwa kuja kubadili katiba baada ya muda mfupi ili ku-accomodate madai ya msingi kabisa ambayo kwa sasa yanapuuzwa au kudharauliwa kwa sababu tu walioyatoa hawaheshimiki au wapinzani au wanaoyakataa wanaona hawana maslahi nayo kwa sasa. Watusaidie na wasituumize kama watanzania tunawaotegemea kututendea mema.
Tisa, wabunge wetu wakumbuke na kuifanyia kazi dhana nzima ya majadiliano yenye kutafuta muafaka. Sayansi ya majadiliano ya kutafuta muafaka inahitaji kusikilizana bila kuchoka. Inahitaji uvumilivu wa mijadala hata pale ambapo inakua migumu sana. Lakini pia inahitaji kila anayeshiriki kwenye meza ya mjadala akubali kuwa atalazimika kupoteza baadhi ya maslahi (interests) yake kwa kukubali baadhi ya maslahi ya anayepingana naye. Kwenye majadiliano hatutumii nguvu na wingi pekee kama kigezo cha maamuzi ya mwisho. Tunatumia mijadala inayoongozwa na nia ya mpende jirani yako kama nafsi yako nay ale upendayo kutendea basin awe mtendee mwenziwe. Nia hii ikiwa ndani mwetu, basi tutakubali baadhi ya madai ya wengine na tutakua radhi kupoteza baadhi ya madai yetu na hivyo mwisho wa siku tukfika panapoitwa muafaka (The open dialogue that leads into consensus). Watanzania hatujajengwa sana katika sayansi ya majadiliano yenye kuzui hisia na miehuko. Lakini hatutegemei sana hata viongozi wetu wawe hawana uwezo huo.
Kumi, yale makundi na wale wabunge wanaoona hawasikilizwi katika hoja ya kupata katiba mpya, wajitahidi sana kutafuta mazingira ya kimjadala. Watumie uwezo na ushawishi wao kutafuta namna amnayo hoja zao zitajulikana, zitasikilizwa, zitaeleweka na zitafanyiwa kazi. Wafanye hivyo wakiwa na nia njema na tayari kuwasikiliza wengine. Wafanye hivyo bila kauli za wao na sisi. Wafanye hivyo kwa sababu wanawajibika na watakua sehemu ya historia ya matokeo ya kitakachopatikana.
Madhara yatakapokuja kujitokeza baadaye kwa hoja zao kutokua sehemu ya mchakato mzima, hakuna atakayewalewa kuwa hayo yametoka kwa kuwa hawakusikilizwa. Watatakikana kutoa ushahidi wa walichokisema kikakatiliwa. Watatakikana kutoa ushaihidi w ajithada zenye nia njema walizochukua na zikakataliwa maana kutuambia tu kuwa walitegemea matokeo mabaya haitakua suluhu ya kuponya matatizo ya kizazi husika.
Mwisho niseme kuwa, wakati wabunge wanapitisha muswada wa kuanzisha mchakato wa katiba mpya, baadhi ya wabunge waligoma kule bungeni; waliulalamikia muswada na kuukataa kwa hoja. Wabunge walio wengi waliwapuuza, waliwaita wajinga, waliwaita wasaliti, wasiotaka katiba mpya, wasio na nia njema na majina mengine kama walivyopenda. Waliwakebehi na kuwaambia ni kawaida yao. Hawakupima uzito wa hoja na uzito wa jambo lenyewe kwa kuona kuwa kwa vile hii ni katima wanalazimika kupata muafaka wa pamoja. Wakaona kura za wingi wao zinatosha kupitisha wanachokitaka.
Ashukuruwe Mungu kuwa Rais wetu (Mzdee Kikwete) aliona kwa jicho la tofauti. Alielewa katiba sio ya wabunge wa chama tawala na serikali yake. Alijua ni ya watanzania na ya wajukuu zake watakaokuwepo baada yake. Tunaweza kusema aliona wabunge wa chama chake wamechemsha na hawakuona mbali vya kutosha na kujikuta wanafanya hata hili kwa mazoea ya ushindani na ushabiki wa kichama. Huenda hakuwaambia lakini mimi nilimwelewa hivyo na kwa hekima yake aliamua kufikisha ujumbe kivingine. Kwa kulidhihirisha hilo alitumia muda wake muhim kukutana na kuwasikiliza wale ambao wabunge wa chama chake kwa wingi wao waliwaona hawana hoja wala hawafai kusikilizwa. Rais aliamua kufanya vikao mwenyewe katika ofisi yake kutafuta muafaka.
Na ni ajabu kuwa yeye mwenyewe alifanikiwa kusikilizana na wenye hoja na wakafikia mahali pa kuelewana. Hakukubali kila hoja iliyoletwa kwake lakini alitafuta muafaka kwa maelezo ya kueleweka. Alitumia uwezo wake mkubwa wa ushawishi katika mzungumzo maana huo ndio uwanja wake wa nyumbani. Unapompa nafasi ya kuzungumza naye ni lazima tu mutafika muafaka (ama wa kukubaliana au kutokukubalina ambako nako ni muafaka).
Nilitegemea wabunge hasa wa chama chake waone aibu hii kubwa na watamani kutorudia tena.
Nilitegemea wajiulize kwa nini walishindwa kuwa na kuona kile alichokiona Rais pamoja na wingi wao. Kwa nini walikosa uvumilivu aliokua nao Mzee Kikwete pamoja na kuwa hakulazimishwa na kanuni wala sheria kufanya lile alilolifanya.
Lakini ajabu ni kwamba leo wabunge wabunge wanamkebehi kile alichofanya Rais huyohuyo bila kujua kuwa wanafanya hivyo. Mzee wa watu alijitosa kuitumia ofisi yake kama mahali sahihi pa kutafuta muafaka wa kitaifa na kimakungi na aliifanya kazi hii bila kukuta tama. Ajabu ni kuwa kazi yake leo inatumika kama kebehi kwa wapinzani kuwa walifuata mandani na chai Ikulu. Ni ajabu kweli. Jitihada ya mkuu wa nchi zinatumika kama kete ya kebehi kwa wapinzani wa kisiasa. Ina maana ni kweli vikao vyote vile Rais alivifanya kama namna ya kuwapa watu maandazi na chain a juice? Ni kweli kuwa taabu yote ile ilikua ni ya kula maandazi? Hapana...mimi ninasema hapana.
Kwa kushindwa kuliona hili wabunge watajikuta wanafanya kosa lilelile la awali na wanaweza kujikuta wanampa Mzee huyu kazi ya kufanya ivkao vingine ama kuwarudishia muswada waujadili upya. Hii ni gharama iyiyo ya lazima na inayoweza kuepukwa na kwa kufanya hivyo heshima ya bunge kama chombo ya majadiliona yenye kuleta muafaka ikatuzwa na kutukuzwa. Wasimpe tena Rais Kikwete kazi ya kuingilia kati maana tayari ana majukumu mengi mengine yanayohitaji sana uwepo na uwajibikaji wake.
Mathew Mndeme
mathewmndeme@gmail.com

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments