[wanabidii] TAMKO LA VUK ZANZIBAR KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA YA TANZANIA BAADA YA KUPITISHWA MABADILIKO YA SHERIA YA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA

Wednesday, September 18, 2013

Vijana wa Umoja wa Kitaifa Zanzibar (VUK) wameguswa na tukio la hivi karibuni katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusiana na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, ambayo ilifanyiwa marekebisho.

Marekebisho hayo yamefanywa huku Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Jaji Joseph Warioba ikianza hatua yake ya kutayarisha Rasimu ya Pili, ambayo itapelekwa katika Bunge la Katiba.

VUK imesikitishwa na mabadiliko hayo ambayo hayakupitia utaratibu wa kushirikisha umma wa Zanzibar, au angalau uwakilishi wa umma, na badala yake kujadiliwa katika ngazi za Serikali tu, yaani Waziri wa Sheria, Mwansheria Mkuu na Baraza la Mapinduzi.

Pia mabadiliko hayo yamepoka uwezo na sauti ya Zanzibar ikiwa ni mshirika mkuu na kamili katika Muungano wa Tanzania kwa kushusha kiwango cha upitishaji wa Katiba na hata vifungu vyake kwa kuweka upitishaji kuwa ya wingi wa "kura za jumla".

VUK inaona hatua mabadiliko hayo ni hatari kwa Zanzibar na hata ni kinyume na kanuni ya kawaida ya kupitisha maamuzi muhimu kama ya masuala ya kikatiba.

Tatu VUK imeshangazwa na uamuzi wa Bunge hilo kupitisha kipengele kinachovunja Tume ya Warioba wakati mchakato ukiwa ndio kwanza mbichi kinyume na ilivyokuwa awali kwamba Tume ya Katiba itavunjika baada ya kupitishwa Katiba Mpya hapo Aprili 2014.

Hatari ya Mabadiliko haya ni kuwa mchakato huo utakuwa hauna mwenyewe wakati wa mjadala, lakini pia mwenyewe atakuwa nani wakati wa Kura ya Maoni hasa itapotokea kuwa kura ya kwanza imekataliwa.

Pili inalekea dhana ya kuivunja Tume ya Katiba inatokana na kuamini kuwa Bunge la Katiba lina uwezo wa kuanza upya kila kitu na hata kubadilisha juu-chini au chini-juu, wakati ukweli ni kuwa kazi ya Bunge la Katiba itakuwa ni kuijadili, kuimarisha na kuikosoa Rasimu ya Pili, ambayo imetarishwa na Tume ya Warioba na kwa hivyo uwepo wa Tume ya Warioba kutoa ufafanuzi, ni wa lazima.

Nne, kulitolewa fikra ya kuzidisha uwakilshi wa uma kutoka watu 166 wataoteliwa na Rais hadi idadi kubwa zaidi ambayo itapunguza nguvu ya wanasiasa katika Bunge la Katiba kwa sababu Katiba inatakiwa iwe ni maridhiano ya umma.

Kwa sababu hiyo basi VUK inamuomba Rais Jakaya Mrisho Kikwete:

. Kwa maslahi ya nchi na kuuokoa mchakato usitoke kwenye reli asitie saini sheria hiyo.

. Rais Kikwete azitake taasisi za Kiserikali zikae na kutizama upya Sheria hiyo na mabadiliko yake mapya kwa kuingia ndani kurudisha kujadiliwa na Wazanzibari

. Kurudisha kipengele cha maamuzi ya 2/3 (thuluthi mbili)

. Kuibakisha Tume ya Warioba hadi mwisho wa mchakato ili kuendelea kutoa muongozi na kusimamia

. Kufikiria mbinu za kuzidisha uwakilishi wa umma.

VUK inavitaka vyama vya siasa na wadau watoe shindikizo lakini pia rai kumsaidia Rais Kikwete juu ya kulifikisha pahala pazuri suala zima la Mchakato wa Katiba ili tusiharibikiwe zaidi.

VUK inawataka vijana wa Kizanzibari wajue hali nzima ya Mchakato wa Katiba unavyokwenda na wakati wowote waunge mkono juhudi za kuwa na utaratibu wa salama hadi kuikamilisha dhamira hiyo.

Pia VUK inawataka Wazanzibari kwa jumla kuwa makini kujua hatua zote za Mchakato wa Katiba zinavyokwenda na kutoa mchango wao kila inapopaswa kwao, maana Zanzibar ina maslahi makubwa katika jambo hili

Salum Abdallah Salum
Kaimu Mwenyekiti
0713742255

USULI:
VUK ni vuguvugu la vijana wa Kizanzibari linalopenda maendeleo na mabadiliko na ambalo linajumuisha vijana wa Kizanzibari wa aina mbali mbali bila ya kujali tofauti zao za kidini, kiitikadi na kimaeneo.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments