[wanabidii] Tahadhari kuhusu uvumi wa “ajira za Wataalamu Jeshini”

Saturday, September 21, 2013
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kuwataarifu Wananchi wote kuwa taarifa zilizoenea kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu za mkononi (sms) na mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba JWTZ limeanza kuajiri wataalamu Jeshini (Professionals) siyo kweli na halina utaratibu wa kutangaza ajira kupitia mitandao ya kijamii au kupitia simu za mikononi. 

Kwa kawaida, utaratibu wa kujiunga na Jeshi hutangazwa kwenye Vyombo vya Habari pale ambapo Jeshi linahitaji kuandikisha askari wapya.  JWTZ huelekeza utaratibu wa kuzingatia katika kuwasilisha maombi husika kwa taarifa hii, wananchi wote wanatahadharishwa kuhusu ujumbe huo unaoelekea kusababisha usumbufu kwa wananchi na JWTZ.  Taarifa hiyo haijatolewa na JWTZ hivyo wananchi wajihadhari na yeyote atakayejitokeza kuwarubuni na hatimaye kutapeliwa kwa namna yoyote.

Imetolewa na: 
Kurugenzi ya habari na Uhusiano 
Makao Makuu ya Jeshi
Dar es salaam, 
Tanzania

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments