[wanabidii] OPERESHENI KIMBUNGA NI MAJANGA

Wednesday, September 18, 2013
"I am not only a Tanzanian or just a Luo, but a citizen of the world...."

Tarehe 16/09/2013 niliitwa Uhamiaji Makao Makuu kwa kisingizio kuwa mimi si raia halali wa nchi ya Tanzania...

Walifuatilia jina langu; wakaangalia na sura yangu eti waka-rule out kuwa mimi si raia wa Tanzania! Wengi wamepata kashi kashi 

hizi hapa mjini na maeneo mengine kama Arusha, Kigoma, Kagera, Musoma, Mwanza, n.k

Wakaniuliza maswali mengi likiwemo hili la kustaajabisha kidogo... Kuwa "Babu mzaa baba yangu au Bibi mzaa mama yangu aliingia 

lini nchini Tanzania...???" Maswali ya kipuuzi nami niliwajibu kipuuzi "Sijuhi kwa sababu sikuwepo kuthibitisha kama ni kweli walitoka 

sehemu nyingine kuingia nchini Tanzania ama la" 

Lakini nami nikawauliza sheria inasemaje kuhusu uraia? - Maelezo niliyopewa hayakuridhisha na ni kiri tu kuwa wale jamaa 

wanaoweka pale ni weupe sana kichwani!

Nikauliza tena swali: Nani ni Mtanzania? Je kama tukianza kuwafuatilia watu kwa asili ya majina yao na maeneo tunayohisi historia 

ndiko ilikoanzia kuna watu watakuwa Watanzania kweli?

Jamani maudhi ya operesheni hii ni mengi sana usiombe yakufikie! Ni waase tu wale wenye majina yenye asili ya nchi kama Kenya, 

Sudani Kusini, Congo DRC, Uganda, Rwanda, Burundi, n.k kamwe usitembee bila vitambulisho vyako - Birth certificate, Voter ID, n.k.

Zoezi hili linaweza kuwa na nia njema kabisa lakini waliopewa kulisimamia na mbinu wazazotumia zitatuachia nyufa nyingi sana na 

uhasama mkubwa sana na majirani zetu! Lakini pia unabaki unajiuliza maswali mengi bila majibu. 

Ina maana hapa nchini usalama wa Taifa hawajui majukumu yao?

Mbona zoezi hili ni kwa baadhi ya watu tu tena waAfrika wenzetu? 

Mbona zoezi linazingatia majina ya watu na muonekano wa sura zao tu? 

Je, ni halali kwa waendesha operesheni kukamata/kugawana mali za watuhumiwa?

Je, taratibu za kidiplomasia zinaelekeza hivi au hizi ni hasira dhidi ya Kenya, Rwanda na Uganda?

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments