Teknologia ya mawasiliano ya simu za mkononi ni kati ya ugunduzi mkubwa sana wa kisayansi ambao umewahi kutokea na kuathiri maisha ya wanadamu wengi kwa wakati mmoja.
Ninadhani utakua ni ugunduzi unafuata baada ya ugunduzi wa kompyuta na mawasiliano ya intaneti. Ugunduzi wa mawasiliano ya simu za mkononi ni matokea ya utafiti wa kisayansi wa karibu karne moja ambao ulifanyika hatua kwa hatua hadi kufikia matokeo tunayoyaona sasa.
Mwanzo wa kizazi (generation) cha simu za mkononi tunazotumia sasa ni kazi mwanasayansi Martin Cooper aliyekua akifanya kazi na kampuni ya Motorola huko Marekani. Simu ya kwanza ya mkononi ambayo mwendelezo wake ndio simu tulizonazo sasa hivi, ilikua ni kubwa na yenye urefu wa kama sentimita 23 hivi na uzito wa kilo moja na gramu mia moja.
Ugunduzi huu ulifanyikwa takribani miaka 40 iliyopitika (1973) lakini hadi sasa mabadiliko makubwa sana ya kitechnologia yametokea sio tu katika kupunguza ukubwa na uzito wa simu ya mkoni, bali pia mfumo mzima wa mitandao ya mawasiliano, matumizi ya mitandao hii na jinsi ilivyounganishwa na mifumo mingine ya

kompyuta na intaneti. Kikubwa zaidi ku kupungua sana kwa gharama za kumiliki simu na tozo la kulipia muda wa mawasiliano.
Hapa kwetu Tanzania, tekonologia hii ilikubalika na kuanza kumumika miaka ya 1990, enzi hizo tukiwa na makampuni kama Traitel na Mobitel (Tigo ya sasa) na hadi sasa tuna makampuni mengi ya simu za mkononi (tunayajua) ambayo mengi yako chini ya sekta binafsi yakishindana katika soko kubwa lenye mamilioni ya wateja.
Ni ukweli ulio wazi kuwa, kama ambavyo imekua katika nchi nyingine nyingi duniani, makampuni ya mawasiliano ya simu za mikononi yamekua na nafasi kubwa sana katika ujumla wa maisha ya watanzania katika nyanja zote za kimaisha. Matumizi ya simu za mkononi ni kati ya huduma za kijamii ambayo imepenya kwa nguvu na kwa sehemu kubwa sana katika maisha ya kila siku ya watu wengi bila kujali ngazi ya elimu waliyonayo, kipato au eneo wanaloishi. Ni ngumu sana kutenganisha huduma za makampuni haya na shughuli za kuichumi, kisiasa, kijamii, taaluma, biashara, kilimo, na nyingine nyingi. Sina haja ya kuelezea umuhim wa huduma za intaneti na fedha zinazotolewa na makampuni haya na jinsi ambavyo kila siku zimetumika kurahisha shughuli za kimaisha.
Kukubalika kwa huduma ya makampuni ya simu na kutumika na mamilioni ya watu, ni wazi kuwa biashara hii inalipa. Ukweli kwamba makampuni ya simu yamekua yakifanya biashara hii kwa miaka mingi sasa na mengine mengi bado yanajiingiza kwenye biashara hii, ni wazi kuwa wanajua wanachokifanya na jamii inaona ni nini makampuni yanafanya. Makampuni haya yamekua wabunifu sana katika kujiendesha na kufanya matangazo ambayo yanamvutia kila mtu na kutamani kujaribisha huduma zinazotolewa; na hii ni afya kwa maelezo yoyote yale yanayoweza kutolewa.
Matatatizo yanayohitaji ufumbuzi
Pamoja na mengi tunayoweza kueleza kuhusu huduma za makampuni ya simu, bado ukweli unabaki kuwa mtumiaji wa huduma hizi au mteja amekua hapewi "hazi zote stahiki" kutokana na kile anachokinunua au kukistahili. Mojawapo kubwa ni mteja kukosa haki ya kujua undani na ukweli wa huduma anazopata pamoja na kuwa na uwezo wa kuhakikisha iwapo alichokilipia ndicho alichokitumia.
Ni kwa muda mrefu sasa kumekua na malalamiko mengi kwa wateja wa simu za mikononi kwa kile wanachokiona kama ni ama kutotendewa haki, kuonewa au kuibiwa na makampuni ambayo kwayo wanapata huduma. Ni mara nyingi tumesikia wabunge na wanasiasa wengine wakipiga kelele kuwa kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za wateja katika matumizi ya huduma za simu za mkononi. Mifano ni mingi ila nitataja michache tu ya kile ambacho kimekua kikillalamikiwa na wateja kwa muda mrefu sasa bila ufumbuzi wa kueleweka:
Ni jambo la kawaida kabisa kwa baadhi ya mitandao ya simu za mikononi kwamteja kuongeza muda wa maongezi kwenye simu yake na baada ya muda kujikuta salio limekwisha au limepungua sana bila kujua lilipotumika au lilivyotumika. Ni mara nyingi wateja wamejikuta wakishindwa kuelewa ni kwa namna gani wamelipia huduma ambazo hawajawahi kuziomba, hawazihitaji wala kujua kuwa wanazo. Sina hakika sana hiki kinaweza kuelezwaje lakini kwa lugha nyepesi na isiyopiga kona nyingi, hiki chaweza kuitwa wizi wa wazi kwa mteja wa huduma za simu za mikononi.
Tatizo liko wapi?
Nini kifanyike?
Pamoja na njia nyingi zinazoweza kutolewa kama suluhisho, kilio kikubwa ni kutaka kuona sheria na vyombo husika, vinachukua hatua za haraka, za makusudi na za uhakika katika kumlinda mtumiaji wa huduma za simu. Kama vile ambavyo vyombo na sheria husika za kibiashara zinatumika vema kulinda makampuni yanayotoa huduma za simu za mkononi, ni haki na wajibu wa vyombo husika kufanya hivyo pia kwa kumlinda mteja ili apate haki zake kwa kile anachokilipia. Wengi wa wateja wa simu ni watu wasio na uwezo wa kifedha wala uelewa wa kutosha kuhusu haki, sheria na wajibu wa watoa huduma na hivyo ni wajibu wa vyombo na sheria husika kuwalinda kama sehemu ya haki zao za msingi za kiraia ndani ya nchi yao. Miongoni mwa mambo ninayoweza kushauri yafanyike ni pamoja na:
Iwapo yatafanya hivyo yalazimishwe kumlipa kwa kila ujumbe wataomtumia kwani wanakua wamemfanya ubao wa matangazo.
---
Mathew Mndeme,
Dar es Salaam, Tanzania

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments