[wanabidii] JESHI LISIJIINGIZE KWENYE MIGOGORO YA ARDHI

Thursday, September 26, 2013
Ndugu zangu 

Kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa tumesikia na kuona jinsi jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ linavyojiingiza kwenye migogoro ya mipaka ya ardhi kati yake na wanavijiji wanaozunguka maeneo hayo hali ambayo imekuwa inatishia usalama wa wananchi husika kwa kuendelea kuishi kwa hofu muda wote .

Kwa maoni yangu nadhani ni wakati wa Jeshi kuwezeshwa au kujiwezesha lenyewe kupitia vitega uchumi vyake kununua ardhi kama kunahitajika kununua ya wanavijiji basi iwe inalipa wanavijiji hao fidia zao kwa wakati na fidia ambayo ni halali kama walivyokubadiliana .

Pia Jeshi lianze kutafuta maeneo mengine ya kuwekeza haswa kwenye shuguli za kilimo , viwanda , utafiti na idara nyingine ili liweze kujipatia kipato kikubwa zaidi liweze kijiendesha kwa faida huku likiajiri maelfu haswa wale waliokaribu na kambi hizo pamoja na kulipa kodi .

Tunapoona Jeshi ambalo ni kama nchi likijiingiza kwenye migogoro ya ardhi na wananchi wanaotegemewa kulindwa jeshi hilo hilo inashangaza kwelikweli .


--
Find Jobs in Africa Jobs in Africa
International Job Opportunities International Job Opportunities
Jobs in Kenya Jobs in Kenya

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments