[wanabidii] Hii ni dharau na fedheha kubwa kwa Taifa

Monday, September 02, 2013

Sinahakika Nilichosikia kama ndicho waziri wa nishati na madini alichokisema akiwa timamu wa akili, huku akimaanisha alichosema. Kama alisema haya        "Watanzania hawana uwezo wa kuwekeza kwenye gesi na mafuta, bali waendelee na biashara ya matunda na juice, na pia hana muda wa kujadiliana chochote na Watanzania  wale wanaofikiria kuwekeza katika mafuta na gesi ".

   Hii ni kauli yake, ya serekali ilitoko madarakani au ya chama chake cha Ccm?
   Kama alizungumza hayo akiwa timamu bila kutumia kilevi chochote wala kuagizwa na Serikali anayoitumikia au chama chake, hakika atakuwa ni mshenzi, mpuuzi na mpumbavu wa mwisho Duniani.                                      Kama si kauli ya Serikali, wala chama chake basi nategemea awajibishwe ipasavyo na mabosi wake kwa kuutukana Umma wa Watanzania na Taifa letu kwa ujumla. Hata kama kweli hatuwezi si lugha ya kuitumia kwa Wananchi wenzako. Lakini siamini kama Serikali ikiweka mazingira rafiki, na sera bora zinazosimamiwa vyema tutashindwa kuwekeza katika gesi na mafuta. Hapa napata wasiwasi na uraia wa ndugu Sospeter Muhogo waziri wa nishati na madini, kwa kauli hii, pia serikali na chama chake.
   Tujithamini, tujipende, tujikubali, tutumie kile tulichonacho kwa faida ya Taifa letu.
  MUNGU IBARIKI AFRIKA MUNGU IBARIKI TANZANIA .

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments