[Mabadiliko] Serikali Tatu Itairudisha Tanganyika, Na Tanganyika Ni Ndoto Ya Wengi Bara..!

Sunday, September 01, 2013

Ndugu zangu,

... Tanganyika si ndoto tu, ni UKWELI wa kihistoria. Na ukweli unaishi. Unapitia hatua 3.
1. Ukiwekwa mezani hukataliwa,
2. Una gharama, kuwa wakati mwingine mwenye kuusema ajiandae kulipa gharama ya kuusema ukweli.
3. Udhihiri, kuwa hata ukifichwa chini ya uvungu wa kitanda kwa miaka 50, iko siku ukweli utatoka hadharani bila kusubiri kuvalishwa viatu. Na uhalali wake uanza kuhesabiwa tangu siku ile ulipokataliwa.

Picha hiyo inaonyesha moja ya nyaraka za tangu mwaka 1993. Waraka huo ( Ninao kwenye maktaba yangu) ulitumwa kwa njia ya Telex kwa balozi zetu duniani kuelezea Azimio la Bunge la wawakilishi wa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutaka kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika. Hata wakati ule, CCM ikaingilia kati, na kwa kupitia vikao vya Chama, ' Ikauficha ukweli huo chini ya uvungu'.

Na hata safari hii ikatokea kwa lazima ukarudishwa tena chini ya uvungu. Bado naamini hoja ya Tanganyika itarudishwa tena mezani, hata baada ya Kingunge na wa kizazi changu kuondoka duniani. Maana, Tanganyika ni UKWELI, ni NDOTO...!
Maggid,
Iringa.

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments