Maana, naamini tukiweza kupata jibu la ' Kwanini?' Basi, tunaweza kupata namna ya kutatua tatizo.
Sababu zaweza kuwa nyingi, lakini kubwa moja ninayoiona ni UJINGA wa hata wale tunaodhani wana uelewa wa mambo, yaweza kuwa ni baadhi ya viongozi wetu, wawe wa kisiasa au hata kidini.
Hawa wanachangia kwa kiasi kikubwa kuwapitisha watu wetu kwenye njia yenye miiba, njia ya hatari. Ni wenye kutanguliza maslahi binafsi kwa mgongo wa siasa za vyama vyao na dini zao pia. Ni hata kwenye mambo ambayo yanaweza kuhatarisha amani na usalama wa nchi.
Naamini, Watanzania tunaweza kuona tofauti kubwa kama tungeamua, kwa mfano, kuwa ndani ya miezi mitatu, yaani siku 90 tu , viongozi wetu wa kisiasa na kidini, kwa pamoja, waamue kutanguliza zaidi masuala ya kitaifa wanapokuwa hadharani, hivyo, ya vyama na dini zao wayafanye kule kunakohusika nayo tu.
Bila shaka, jaribio kama hilo lingetuonyesha Tanzania nyingine inayowezekana. Maana, leo hata maafa kama haya ya aibu, ya watu kumwagiwa tindikali na mengineyo, yanapewa sura za kisiasa na kidini. Hivyo basi, kuwasaidia zaidi wahalifu kuliko raia wema wa nchi. Inaonyesha tusivyoshikamana kama taifa.
Katika kama haya ya kishenzi ya raia na hata raia wa kigeni kumwagiwa tindikali, tungetarajia viongozi wakuu wa kisiasa , bila kujali tofauti zao za kiitikadi, wawe wanatoka haraka kwa pamoja na kutoa matamko ya pamoja. Hivyo hivyo kwa viongozi wakuu wa kidini, bila kujali tofauti zao za kidini. Watoke na watoe matamko ya pamoja.
Iwe hivyo badala ya hali ya sasa, ya kila linapotokea baya la kitaifa, kuna viongozi wa kisiasa na kidini wenye kuyakimbilia na kuyatolea matamko yanayobeba sura za rangi za vyama vyao na sura za dini zao.
Naam, Hiii Ni Nchi Yetu. Ni nchi yetu sote. Tuwe na ujasiri wa kukubali, kuwa Nchi ni kama nyumba kubwa tunayoishi sote, kama familia. Hivyo, kama kuna nyoka ameingia kwenye nyumba tusianze kuulizana maswali ya; ana urefu gani? Ana rangi gani? Wa dini gani? Kamleta nani? Na kadhalika.
Nyoka ni nyoka tu. Kwa pamoja na kwa kutanguliza maslahi ya nchi yetu, tuna lazima ya kupambana na nyoka huyo ili tubaki salama. Tufanye hivyo kama Nchi na kama watu wa familia moja. Watu tunayoishi kwenye nyumba moja.
Asubuhi Njema.
Maggid.
Dar es Salaam.
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments