Ndugu zangu,
Ulimwengu umepatwa na mshtuko mkubwa kwa kuona picha za tukio kubwa la kigaidi kwenye moja ya maduka makubwa jijini Nairobi. Hili ni shambulio kubwa la kigaidi kupata kutokea Afrika Mashariki tangu lile la mwaka 1998. Na ajabu ya kihitoria ni kuwa matukio mengi ya kigaidi yametokea katika mwezi wa Septemba.
La Nairobi ni shambulizi la kigaidi la kulaaniwa vikali na wapenda amani wote ulimwenguni.
Hata hivyo, moja ya tafsiri ya vitendo vya kigaidi tunavyovishuhudia Nairobi ni kuwepo kwa hali ya vita vya kigaidi vyenye kuendeshwa kwenye maeneo ya mijini (Urban terrorism).
Ni shambulizi lenye athari mbaya kiuchumi si tu kwa nchi ya Kenya, bali hata majirani zake ikiwemo Tanzania. Ni shambulizi lililowaogopesha wageni wengi wakiwamo wawekezaji pia. Kwamba Al Shabaab inalenga pia nchi za Magharibi. Hivyo basi, hata raia wake. Kunahitajika jitihada za pamoja kuwaondoa hofu watu wa mataifa ya nje, kuwa kilichotokea Nairobi kitadhibitiwa kwa njia zote, kisitokee tena.
Na hakika, aina hii ya ugaidi ni ngumu sana kudhibitika hatakama nchi ina jeshi kubwa na lenye vifaa vya kisasa. Inahitaji ushiriki wa raia wema katika kutoa taarifa za wahalifu hata kabla hawajafanya matendo yao maovu. Inahitaji pia maandalizi makini, ya kuwa na vikosi vilivyo tayari wakati wote kukabiliana na matukio kama haya.
Ni dhahiri, kuwa mbinu inazotumika kikundi cha kigaidi cha Al Shaabab ambacho maana hasa ya jina hilo ni ' Vijana', ni moja ya changamoto kubwa katika mapambano dhidi ya ugaidi.
Al Shabaab iliundwa mwaka 2006. Kinasemekana kuwa na wapiganaji wenye silaha wapatao 10,000. Al Shabaab katika miaka ya karibuni wamepoteza maeneo mengi ya mijini waliyokuwa wakiyadhibiti, ikiwamo mji wa Kismayu ambao majeshi ya Kenya yaliudhibiti baada ya kuwasambaratisha Al Shabaab. Kwa sasa Al Shabaab bado wana nguvu maeneo ya vijijini katika Somalia.
Kufuatia Kenya kujiingisha kijeshi kupanbana na Al Shaabab, kikundi hicho kimeifanya Kenya kuwa adui na kutangaza wazi azma yake ya kuishambulia Kenya. Mwezi Aprili mwaka huu watu watano walipoteza maisha nchini Kenya baada ya wapiganaji wa Al Shabaab kuingia kwa nguvu wakiwa na silaha kwenye mgahawa mmoja kwenye mji wa Garissa nchini Kenya.
Mwaka 2012 ndipo Al Shabaab walipojiunga rasmi na mtandao wa kigaidi wa Al qaida chini ya kiongozi wa Al qiada, Aymab al- Zawahiri.
Maggid,
Iringa.
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments