Wakala wa Mbegu za Miti
(Tanzania Tree Seed Agency –TTSA)
UANZISHWAJI, MAFANIKIO NA CHANGAMOTO
Ludovick Uronu
Kaimu Mtendaji Mkuu
Wakala wa Mbegu za Miti
Mada iliyotolewa kwa waandishi wa habari Dar es Salaam, 29 Agosti 2013
1.1 HISTORIA YA UANZISHWAJI WA WAKALA WA MBEGU ZA MITI TANZANIA
1.1.1Hali ya misitu Tanzania
Eneo lote la misitu Tanzania ni Hekta 48 millioni (Ekari 119 millioni), kati ya hizo 96% ni msitu mataji wazi (woodland), 0.3% ni misitu ya mikoko (mangrove) na 3.4% ni misitu mingineyo.
Katika eneo lote la misitu ni 33% tu ndiyo zipo katika hifadhi ya misitu kisheria. Uharibifu wa misitu Tanzania unakadiriwa kuwa hekta 412,000 kwa mwaka. Uharibifu huu unatokana na ukataji wa miti kiholela ,uchomaji moto ovyo wa misitu, idadi ya mifugo inayozidi uwezo wa eneo ,Kilimo cha kuhamahama, maendeleo ya viwanda na ujenzi wa makazi .
Athari zinazotokana na upungufu wa misitu ni: kusababisha mmmomonyoko wa udongo, uchafuzi wa hewa na maji, kuongezeka kwa joto la dunia na upungufu wa mazao ya misitu. Ukarabati wa maeneo ya misitu yaliypharibika unakisiwa kuhitaji takribani miche ya miti milioni 440 kwa mwaka sawa na wastani wa tani 40 ya mbegu za miti kwa mwaka
1.1.2 Historia fupi ya uzalishaji wa mbegu za miti Tanzania
v Uzalishaji ulianza wakati wa utawala wa Mjerumani chini ya Taasisi ya Kibaiyolojia na Kilimo iliyokuwa imeanzishwa na Wajerumani mwaka 1902 huko Amani Mkoa wa Tanga
v Mbegu za wakati huo zilikuwa ni aina ya Misindano (Pinus spp.), Misanduku (Cupressus spp.) na Mikaratusi (Eucalyptus spp.)
Mwaka 1951 serikali ilianzisha kituo cha Utafiti wa Misitu (Silviculture v Research Station) huko Lushoto, mkoa wa Tanga mwaka 1951.
v Kituo hicho kilikuwa na kitengo cha mbegu za miti kilianzishwa kwa madhumuni ya kuzalisha na kusambaza mbegu za miti kwa ajili ya utafiti na mashamba ya miti ya serikali.
v Miaka ya 1970 serikali ya Tanzania ilianzisha mpango wa kitaifa wa kupanda miti ili kuboresha mazingira ambayo yalikuwa yameharibika pamoja na mahitaji mengine
Kituo cha Utafiti wa Misitu Lushoto, hakikuweza tena kumudu mahitaji hayo kwa sababu ya kijiografia (kiko pembezoni mwa nchi, mbali na v wateja wa mbegu) pia hakikuwa na vitendea kazi vya kutosha.
v Serikali ya Tanzania ilitambua changamoto hiyo na ndipo ilibuni Mradi wa Taifa wa Mbegu za Miti (National Tree Seed Programme – NTSP), chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii mwaka 1989 wenye makao makuu mjini Morogoro.
v NTSP ilikuwa na majukumu ya kuzalisha na kusambaza mbegu bora za miti ili kukidhi mahitaji ya humu nchini na kuuza ziada nchi za nje
Kufuatana na programu ya serikali ya kuboresha utumishi wa umma (Public Service reforms programme), NTSP ilibadilishwa kuwa Wakala v wa Mbegu za Miti (Tanzania Tree Seed Agency – TTSA).
- WAKALA WA MBEGU ZA MITI
TTSA yenye makao makuu yake mjini Morogoro, ni Wakala wa Serikali unaofanya shughuli zake chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii. TTSA ilizinduliwa tarehe 24 Januari 2003 chini ya sheria ya Wakala za Serikali Na. 30 ya mwaka 1997. Madhumuni ya TTSA ni ''Kuwezesha upatikanaji endelevu wa mazao ya misitu na utunzaji wa mazingira nchini kwa kuzalisha na kusambaza mbegu bora za miti pamoja na vipandikizi vingine".
2.1Vyanzo vya mapato vya TTSA
2.1.1 Mbegu za miti
Chanzo kikubwa cha mapato ya TTSA ni kuuza mbegu bora za miti.TTSA inakusanya na kuuza mbegu bora za miti ndani na nje ya nchi. Wastani wa tani 12.5 ukusanywa na kuuzwa kila mwaka ndani na nje ya nchi. Nje ya nchi TTSA inauza mbegu za miti katika nchi za Msumbiji, Afrika Kusini, India, Vietnam, Guatemala, Rwanda, Uganda, Australia, Botswana, Singapore , Ufaransa, Marekani, Madagascar, Siera leone, Denmark, Costa Rica na Malawi.
Aina za mbegu za miti zilnazouzwa ni 195 na kati ya hizo, aina za miti ya kienyeji ni asilimia 60 iliyosalia ni mbegu za miti ya kigeni. Mbegu zinazoongoza kwa kupendwa katika soko ni Mkangazi (Khaya anthotheca), Mtiki (Tectona grandis), Mwerezi (Cedrela odorata), Mkenge (Albizia lebbeck), na Mkongo (Afzelia quanzensis), Msindano (Pinus patula), Mtikivuli (Acrocarpus fraxinifolius).
2,1.2 Miche ya miti
Chanzo kikubwa cha mapato ya TTSA ni kuuza mbegu bora za miti.TTSA inakusanya na kuuza mbegu bora za miti ndani na nje ya nchi. Wastani wa tani 12.5 ukusanywa na kuuzwa kila mwaka ndani na nje ya nchi. Nje ya nchi TTSA inauza mbegu za miti katika nchi za Msumbiji, Afrika Kusini, India, Vietnam, Guatemala, Rwanda, Uganda, Australia, Botswana, Singapore , Ufaransa, Marekani, Madagascar, Siera leone, Denmark, Costa Rica na Malawi.
Aina za mbegu za miti zilnazouzwa ni 195 na kati ya hizo, aina za miti ya kienyeji ni asilimia 60 iliyosalia ni mbegu za miti ya kigeni. Mbegu zinazoongoza kwa kupendwa katika soko ni Mkangazi (Khaya anthotheca), Mtiki (Tectona grandis), Mwerezi (Cedrela odorata), Mkenge (Albizia lebbeck), na Mkongo (Afzelia quanzensis), Msindano (Pinus patula), Mtikivuli (Acrocarpus fraxinifolius).
2,1.2 Miche ya miti
TTSA inazalisha na kuuza miche ya miti kwa ajili ya matumizi mbalimbakama mbao, nguzo, mkaa, kuni, madawa, mapambo, kilimo mseto, kivuli na hifadhi ya maji. Pia TTSA inazalisha miche bora ya miembe na michungwa ambayo inazaa matunda kati ya miaka miwili hadi mitatu baada ya kupandwa. Aina ya miembe inayozalishwa ni Tommy Atkin, Kent, Keitt, Red Indian, Dodo, Sensation, Alphonso, Apple na Julie. Aina za michungwa ni Valencia, Parson brown, Matombo sweet, Jaffa na Orlando.
2.1.3 Kumbi za mikutano
Wakala unazo kumbi tatu za mikutano ambazo zinakodishwa, taasisi za serikali ndio wateja wakubwa kutokana na kumbi hizo kuwa katika mazingira mazuri na ya utulivu na uwepo wa "standby generator".
2.1.4 Mafunzo ya muda mfupi
Wakala unaendesha mafunzo ya muda mfupi ya uanzishaji na uendelezaji wa bustani ya miche ya miti mara mbili kila mwaka, Aprili na Oktoba.
2.1.5 Ushauri wa kitaalamu (Consultancy)
Wakala unatoa ushauri wa kitaalamu katika Nyanja mbalimbali za misitu, kama utambuzi wa mimea, kuboresha mazingira (Landscaping) na kukarabati maeneo ya misitu yaliyoharibiwa (Forest rehabilitation).
3. MAFANIKIO NA CHANGAMOTO
3.1 Mafanikio
3.1.1 Kiasi cha mbegu na miche iliyosambazwa humu nchini
Mwaka | Kiasi cha mbegu (kg) | Idadi ya miche |
2003 | 7,250 | 9,750 |
2004 | 8,300 | 10,150 |
2005 | 11,252 | 12,852 |
2006 | 9,587 | 32,215 |
2007 | 10,165 | 41,698 |
2008 | 9,637 | 179,670 |
2009 | 10,136 | 194,619 |
2010 | 12,300 | 61,780 |
2011 | 12.400 | 64.200 |
2012 | 3,954 | 47,016 |
2013 | 20,245 | 38,772 |
Jumla | 102,838 | 628,586 |
Kiasi cha mbegu na miche iliyosambazwa na TTSA katika kipindi cha miaka 10 (2003 – 2013) kinaweza kwa wastani kutosha kupanda Ha 643,131 (Ekari 1,588,534) za misitu. Kwahiyo ufanisi wa TTSA hauwezi kupimwa kwa mapato pekee bali kwa kiasi inachochangia katika kuboresha mazingira nchini. TTSA ni moja kati ya Wakala za serikali ambazo zinatoa huduma na kufanya biashara.
3.2.1 Mapato na "Sustainability" katika kipindi cha miaka kumi (2003 – 2013)
Mwaka | Mapato ya TTSA | Mchango wa Serikali (PE + OC) | Jumla | TTSA Sustainability |
2003/2004 | 131,621,570 | 322,245,913 | 453,867,483 | 29% |
2004/2005 | 182,280,991 | 405,722,206 | 588,003,197 | 31% |
2005/2006 | 245,896,401 | 328,858,095 | 574,748,496 | 43% |
2006/2007 | 359,422,408 | 315,359,104 | 674,781,512 | 53% |
2007/2008 | 327,906,170 | 320,210,671 | 648,116,841 | 51% |
2008/2009 | 337,067,686 | 453,664,265 | 790,731,951 | 43% |
2009/2010 | 426,169,954 | 453,203,302 | 879,373,256 | 48% |
2010/2011 | 338,574,949 | 589,186,785 | 927,761,734 | 36% |
2011/2012 | 186,736,420 | 579,419,000 | 766,155,420 | 24% |
2012/2013 | 472,144,267 | 499,676,110 | 971,820,377 | 49% |
3.1.3 Vyanzo vya mbegu bora
TTSA ina vyanzo 385 vya mbegu. Vyanzo hivyo vipo maeneo mbalimbali ikiwemo katika hifadhi za misitu. TTSA imeendelea kuboresha vyanzo vya mbegu pamoja na kuanzisha vyanzo vipya vya mbegu kutokana na mbegu zilizoboresha ili kuendelea kupata mbegu bora zaidi.
Baadhi ya vyanzo vya mbegu vilivyoboreshwa ni:Mtiki (Tectona grandis),Msindano (Pinus patula), Mkaratusi (Eucalyptus grandis),Mkaratusi (Eucalyptus tereticornis), Mkorimbia (Corymbia citriodora,)Mgrevilea (Grevillea robusta),Mvule (Milicia excelsa), Mninga (Pterocarpus angolensis),Mwarobaini (Azadirachta indica), Mtiki mweupe (Gmelina arborea,)na Mgliricidia (Gliricidia sepium).
3.1.4 Mafunzo mafupi ya Uanzishaji na Uendelezaji wa Bustani ya vitalu vya miti
Katika kipindi cha miaka 10 TTSA imetoa mafunzo mafupi ya uanzishaji na uenelezaji wa bustani za vitalu vya miti kwa washiriki 400 katika mikoa ya Arusha, Dodoma, Dar es Salaam, Iringa, Morogoro, Kilimanjaro, Mtwara, Pwani, Mara, Mwanza, Tanga, Kigoma, Tabora, Singida, Shinyanga, Pemba na Unguja.
3.1.5 Ushauri wa kitaalamu (Consultancy)
TTSA imetoa ushauri wa kitaalamu wa tambuzi wa mimie ya aslili na ushauri wa mimea ya kuboresha mazingira (Rehabilitation) katika makampuni manne ya migodi ya dhahabu ya Geita Gold Mine, Tulaweaka Gold Mine, Resolute Tanzania na North Mara Gold Mine pia Kiwanda cha Cement Tanga. Pia imetoa ushauri wa uanzishaji na uendelezaji wa bustani za vitalu vya miche kwa wadau mbalimbali wa miradi ya upandaji miti.
3.1.5 Ajira
TTSA imefanikiwa kuajiri jumla ya watumishi 30 wapya wa kada mbalimbali mara mbili baada ya kupata kibali cha ajira.
3.1.7 Wafanyakazi waliojiendeleza kielimu
Tangu 2003 hadi 2013 TTSA ilipoanzishwa baadhi ya wafanyakazi wamejiendeleza kielimu na wakahitimu katika ngazi mbalimbali kama ifuatavyo:
· PhD (Biology) ---------------------------------- 1
· MSc. (Forestry) ------------------------------- 1
· MSc. (Seed Conservation) ----------------- 1
· BSc. (Forestry) -------------------------------- 2
· BA (Human Resource) ---------------------- 1
· Adv. Diploma (IT) ----------------------------- 1
· Diploma (Secretarial Studies) ------------- 1
· Certificate (Forestry) ------------------------- 6
3.1.8 Wafanyakazi walioko masomoni ni kama ifuatavyo:
· MBA (Human Resource) ------------------- 1
· MAB (Corporate Management)-------------- 1
· BSc. (Forestry) -------------------------------- 2
· Bachelor Degree (Accoutancy)------------- 1
· BSc. (Lab. Science) -------------------------- 1
· Diploma (Forestry------------------------------- 1
3.1.7 Wadau wanaofaidika moja kwa moja na huduma za TTSA:
Miradi ya serikali inayojihusisha na upandaji miti
Mashirika ya siyo ya kiserikali yanayojihusisha na upandaji miti
Halmashauri za Wilaya,
Mashamba ya miti ya wawekezaji
Watu binafsi wenye bustani za miche,
Wanavijiji na wakulima.
3.1.9 Ushirikiswaji wa umma
v Karibu ya 1/3 ya mashamba ya mbegu ya TTSA yapo katika ardhi inayomilikiwa na wananchi.
v Mbegu zinazokusanywa hatimaye husambazwa kwa wananchi kupitia wakala za serikali na mashirika yasiyo ya kuserikali ambao ni wateja wa TTSA.
v Wananchi wanashirikishwa katika ukusanyaji wa baadhi ya mbegu za miti chini ya usimamizi wa wataalamu wa TTSA na hulipwa kwa kazi hiyo. Hivyo hupata pesa na kuboresha maisha yao.
3.1 CHANGAMOTO NA UFUMBUZI WAKE
3.2.1 Upungufu wa Wafanyakazi
- TTSA inawafanyakazi 53 tu ukilinganisha na 128 ambao ndio wanaotakiwa.
- Kila mwaka TTSA inaajiri watumishi wapya baada ya kupata kibali kutoka serikalini.
- Ni matumaini yetu kuwa miaka michache ijayo wakala utakuwa na watumishi wa kutosha.
- TTSA inatarajia kushirikiana na watu wenye maduka ya pembejeo za kilimo kusambaza mbegu kwa kutumia vifuko vidogo.
3.2.2 TTSA ni ndogov TTSAS ni ndogo sana ukilinganisha na ukubwa wa nchi yetu.v Tunayo mpango wa kuanzisha kituo cha nne cha Kanda ya Ziwa huko katika jiji la Mwanza kwa ajili ya kuhudumia mikoa mitano inayozunguka ziwaVictoria.v TTSA inafanya mchakato wa kuchagua watu binafsi wa kusambaza mbegu za miti katika mikoa sita.v TTSA inatarajia kuwatumia watu hao kusambaza mbegu kwa kutumia vifuko vidogo.v TTSA inashirikiana na Chuo Kikuu cha Copenhagen katika mpango huu wakutumia vifuko vidogo.3.2.3 Uwezo mdogo wa watejav Wateja walio wengi wana uwezo mdogo kifedha hivyo wanalalamika kuwa bei za mbegu ni kubwa.v TTSA inajitahidi kutoongeza bei za mbegu.v Kuuza mbegu katika mifuko midogo kutapunguza tatizo hili kwa kiasi.3.2.4 Kutojulikana sawasawav Watu wengi bado hawajui kuwepo kwa TTSA.v Mkakati wa TTSA ni kujitangaza katika vyombo vya habari (magazeti, radio, vipeperushi, TV, mabango n.k)v Pia tunatembelea wateja wetu mara kwa mara na kushiriki katika maonyesho ya kimataifa sabasaba na kitaifa nanenane.3.2.4 Mchango mdogo kutoka serikalini-
- Kila mwaka TTSA inapoandaa bajeti hushauriwa na serikali iipunguze.
- Kuna miaka ambapo pesa zilizoidhinishwa hazitolewi zote.
- Hili ni eneo mojawapo ambalo tunahitaji wahisani.
4. MAJUMUHISHO- TTSA inajivunia kuwa na mazingira mazuri ya kufanyia kazi. Pia serikali huwa inateua Bodi ya Ushauri (Ministerial Advisory Board-MAB) yenye Mwenyekiti na wajumbe wenye busara ambao wanateuliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii. TTSA pia ina wafanyakazi mahiri wenye taaluma zinazotakiwa, wanaojituma na kuwajibika.
- Hii ndiyo maana TTSA ni mojawapo ya taasisi bora za mbegu za miti katika Afrika.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments