[wanabidii] Ufafanuzi wa Wizara kuhusu habari ya Nipashe “Elimu: Aibu, aibu”

Monday, August 05, 2013
Picture

YAH: UFAFANUZI KUHUSU HABARI ILIYOANDIKWA KATIKA GAZETI LA NIPASHE LA TAREHE 05 AGOSTI, 2013 INAYOSOMEKA "ELIMU: AIBU, AIBU"

 
Katika gazeti la Nipashe la leo Jumatatu tarehe 5 Agosti, 2013 toleo Namba 057834 ukurasa wa mbele na wa nne kuna habari inayosomeka"Elimu: Aibu, aibu". Katika habari hii mwandishi anaelezea kwamba kuna Madudu zaidi yamebainika katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, baada ya kuwapanga baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tano kwenye shule ambazo hazina masomo ya michepuo yao.
 
Habari hiyo imenukuliwa kimakosa kutoka katika Tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambapo
imepotosha ukweli wa Taarifa husika. Usahihi wa Taarifa yenyewe ni kwamba wanafunzi waliobadilishiwa shule ni wale walioomba wenyewe kubadilishiwa michepuo (combination) na si kwamba walibadilishwa kutokana na kukosa michepuo waliyopangiwa awali katika shule hizo.
 
Aidha, wanafunzi wengine waliobadilishiwa shule ni wale waliopangwa mbali kutoka sehemu wanazoishi, walio wagonjwa wanaohitaji kuwa karibu na hospitali na walioomba kupangwa katika shule za kutwa kutokana na sababu za kiuchumi.
 
Wizara huwapanga wanafunzi wa Kidato cha tano kwa kufuata Taarifa zilizojazwa na wanafunzi wenyewe kwenye Selection Form (SEL Form)ambapo wanafunzi wanajaza machaguo yao kulingana na matarajio yao.
 
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilitangaza matokeo ya kupangwa Kidato cha 5 wanafunzi waliohitimu kidato cha 4 mwaka 2012 tarehe 10 Julai, 2013. Baada ya tangazo hilo, Wizara ilipokea maombi ya wanafunzi wanaotaka kubadili shule au machaguo (combinations) walizopangwa kwa sababu mbalimbali. Wizara ilitafakari maombi hayo na kufanya mabadiliko ya shule/ machaguo.
 
Imetolewa na:
Ntambi Bunyazu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
 
05/08/2013

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments