Historia inatufundisha kuwa kuanzia enzi za ukoloni ( dutch ostafrica) nchi yetu ilikuwa imezunguukwa na maadui. Rwanda na Burundi baadae wakatolewa na tukajiunga na wisiwa ambavyo pia vilikuwa chini ya himaya ya maadui zetu. Leo chokochoko zote hizo tunaziona pande zote magharibi,mashariki, kaskazini na kusini mwetu (Malawi). Enzi za Mwl. Nyerere tulikuwa na chama kimoja tu, leo tuna vyama vingi, hiyo sauti zimekuwa nyingi kiasi kwamba zinaleta chuki kwa baadhi yetu. Wanaotawala hawataki kukoselewa na wapinzani wao, kwa njia hiyo umoja mnaosema ndio unaonekana haupo. Hayo ni baadhi tu ya matokea ya demokrasia.
Tunachotakiwa sisi kufanya ( especially for us intelectuals) sio kuwakosoa viongozi wetu katika masuala ya kimataifa. Hayo ya ndani tunaweza kukosoana sana. Kwa mfano,kusema kuwa hatuwezi kushinda vita hata kanakwamba tuna jeshi kubwa kunamuongezea jeuri Mnyarwanda ambaye atasoma tuuandikavyo. Umoja ni sisi sote tunapaswa kuuimarisha. Tuna methali nyingi zinazo ongelea umoja, kidole kimoja hakivunji chawa.
Mtanganyika
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments