UTANGULIZI
Mfuko wa Pensheni wa PPF ni Mfuko mkongwe hapa nchini, ulianzishwa mwaka 1978 kwa Sheria ya Mfuko wa Pensheni wa PPF Sura na. 372 kwa madhumuni ya kutoa mafao ya pensheni na mafao mengine yanayoendena na hayo kwa wafanyakazi wote walio katika sekta rasmi na zisizo rasmi.
MAJUKUMU YA MFUKO
PPF ina majukumu yafuatayo:-
i) kuandikisha wanachama,
ii) kukusanya michango,
iii) kuwekeza michango inayokusanywa na
iv) kulipa mafao ya pensheni na mafao mengine yanayoendana na hayo kwa wanachama wake.
WIGO WA UANACHAMA
Mfuko unaandikisha wanachama kutoka katika sekta zote za uchumi mashirika ya umma, makampuni binafsi,

waliojiajiri wenyewe na sekta isiyo rasmi
Mafao ya PPF: Mfuko wa PPF una mafao saba baadhi ya mafao ambayo Mfuko unatoa ni
UWEKEZAJI
Jukumu linginge kubwa ni kuwekeza; Mfuko wa PPF unawekeza kwa mujibu wa sera ya uwekezaji sambamba na mwongozo wa uwekezaji wa SSRA na BOT. Baadhi ya sehemu Mfuko unawekeza katika
MAFANIKIO YA MFUKO
IDADI YA WANACHAMA
Mfuko umeendelea kukua kwa upande wa uanachama ambapo hadi kufikia mwezi Juni 2013, tulikuwa na jumla ya wanachama 224,193 ukilinganisha na wanachama 203,981 kwa mwezi Desemba 2012
Vile vile Mfuko umepunguza matumizi ya karatasi yaani 'paper work' kwa kurahisisha malipo kwa wanachama na kwa upande wa watoa huduma tunatumia mfumo wa 'E-banking' yaani pesa zinatumwa moja kwa moja kwenye akaunti ya mhusika.
Kupitia mifumo ya kisasa ya PPF, mwanachama anaweza kupata taarifa zake za michango, dai au pensheni kwa mstaafu kupitia simu ya kiganjani au tovuti ya Mfuko ambayo ni www.ppftz.org Mwanachama anaandika neno michango anaacha nafasi anaweka namba ya uanachama na kutuma kwenye namba 15553. Si hivyo tu , bali hata mwajiri anaweza kupata taarifa za michango ya wafanyakazi wake akiwa katika sehemu yake ya kazi bila kwenda katika ofisi za PPF hii inaokoa muda na pia kuongeza uhakika wa uwasilishwaji wa michango ya wanachama.
Kwa kutambua umuhimu wa matumizi ya mifumo ya habari mwaka huu 2013 katika wiki ya Hifadhi ya Jamii, Mfuko wa Pensheni wa PPF ulitunukiwa hati ya utambuzi kama Mfuko bora kwenye matumizi ya Mifumo ya habari. Hati hiyo ilitolewa na Mhe. Rais, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,kwa kuwa Mfuko bora katika Nyanja ya mifumo ya habari kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwenye kutoa huduma mbalimbali.
Tunatoa mikopo hii kupitia SACCOS za wanachama wetu zilizopo kwenye maeneo yao ya kazi.
Mpaka sasa tumeshatoa zaidi ya Billioni 56 kwenye SACCOS 46
Tumewekeza kwenye ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwa ajili ya kuwauzia wanachama wetu.PPF imekuwa Mfuko wa kwanza kwa kuanzisha miradi ya nyumba za bei nafuu.
Tulijenga nyumba 580 Kiseke Mwanza na tuliziuza kwa bei nafuu ya kati ya shilingi millioni 16 mpaka million 33. Zoezi hili ni endelevu kwa mikoa mingine
LENGO
Katika Mpango mkakati wa Mfuko kwa kipindi cha miaka 3 (2013-2015) baadhi ya malengo ya Mfuko ni kama ifuatavyo:
Mwisho kabisa ningependa kuwashukuru wanachama na wadau wote wa Mfuko kwa Mchango Mkubwa Mliotupa.
Hivyo tunaomba tuendelee kushirikiana kwa kuendelea kuwa wanachama wa PPF na wale ambao bado hamjajiunga na PPF tunaomba mjiunge ili muweze kuwa na uhakika wa maisha yenu ya sasa na baadaye.
Asanteni
Lulu Mengele
Meneja Uhusiano na Masoko
Mfuko wa Pensheni wa PPF
Simu: 0782 249994

- Mafao ya Pensheni ambapo hutolewa pale ambapo mwanachama anapokuwa amechangia kwa kipindi cha miaka 10 au zaidi na amefikia umri kustaafu yaani miaka 55 mpaka 60.Na awe ameondoka kwenye ajira. Mpaka sasa PPF ina wastaafu wapatao 25,896 na tunalipa kila mwezi Billioni 3.7. Hii ni kwa mafao ya uzeeni tu mnaweza kuona jinsi tunavyosaidia kuondoa umaskini na kukuza uchumi wa nchi.
- Mafao ya Ugonjwa: Hutolewa pale ambapo mwanachama wa PPF anapokuwa ameondoka kazini kwa sababu za ugonjwa na imedhibitishwa na Daktari kwamba kweli hawezi kufanya kazi tena
- Mafao ya Elimu: Hutolewa pale ambapo mwanachama wa PPF anapokuwa amefariki dunia baada ya kuchangia kwa muda wa miaka 3 au zaidi. Fao hili hutolewa kwa watoto wa mwanachama wasiozidi 4 kwa kulipia gharama ya elimu ya chekechea mpaka kidato cha nne. Kwa kutambua umuhimu wa elimu kuanzia mwakani 2014 Mfuko unaongeza muda wa kuwasomesha watoto mpaka kidato cha sita. Tunalipa mmoja kwa mmoja kwenye shule za watoto wanachama
UWEKEZAJI
Jukumu linginge kubwa ni kuwekeza; Mfuko wa PPF unawekeza kwa mujibu wa sera ya uwekezaji sambamba na mwongozo wa uwekezaji wa SSRA na BOT. Baadhi ya sehemu Mfuko unawekeza katika
- Majengo kama vile ofisi mfano PPF Tower,PPF Plaza Mwanza,vile vile wekeza kwenye hoteli,nyumba za kupanga vile vile tume tumeshiriki kwenye ujenzi wa vyuo vikuu kama vile UDOM-kwenye chuo cha Mifumo ya Komputa na chuo kikuu cha sayansi na Teknologia Nelson Mandela kilichopo Mkoani Arusha.
- Tumeshiriki kwenye uwekezaji katika sekta ya Kilimo Kagera Sugar, 21st Century kiwanda cha Nguo Morogoro
- Uwekezaji mwingine ni kwenye Mikopo ya Saccos kwa wanachama wetu ambapo PPF unakopesha wanachama kwenye maeneo ya Kazi ambapo inasaidia kukuza uchumi
MAFANIKIO YA MFUKO
- Mfuko umetimiza miaka 35 mwaka huu na ulianza kwa mtaji wa shilingi million 50 mwaka 1992.lakini Mfuko unaendelea vizuri kwa kuwa na uwezo wa kulipa mafao kwa wakati bila kulazimika kuuza vitega uchumi au kukopa mahali popote
- Kwa upande wa thamani ya Mfuko: Mfuko umeendelea kukua mwaka hadi mwaka ambapo kwa sasa thamani ya Mfuko ni shilingitrillion 1.3 ukilinganisha na mwaka jana 2012 Desemba ambapo thamani ya Mfuko ilikuwatrillion 1.09
IDADI YA WANACHAMA
Mfuko umeendelea kukua kwa upande wa uanachama ambapo hadi kufikia mwezi Juni 2013, tulikuwa na jumla ya wanachama 224,193 ukilinganisha na wanachama 203,981 kwa mwezi Desemba 2012
- Matumizi ya mifumo ya habari:
Vile vile Mfuko umepunguza matumizi ya karatasi yaani 'paper work' kwa kurahisisha malipo kwa wanachama na kwa upande wa watoa huduma tunatumia mfumo wa 'E-banking' yaani pesa zinatumwa moja kwa moja kwenye akaunti ya mhusika.
Kupitia mifumo ya kisasa ya PPF, mwanachama anaweza kupata taarifa zake za michango, dai au pensheni kwa mstaafu kupitia simu ya kiganjani au tovuti ya Mfuko ambayo ni www.ppftz.org Mwanachama anaandika neno michango anaacha nafasi anaweka namba ya uanachama na kutuma kwenye namba 15553. Si hivyo tu , bali hata mwajiri anaweza kupata taarifa za michango ya wafanyakazi wake akiwa katika sehemu yake ya kazi bila kwenda katika ofisi za PPF hii inaokoa muda na pia kuongeza uhakika wa uwasilishwaji wa michango ya wanachama.
Kwa kutambua umuhimu wa matumizi ya mifumo ya habari mwaka huu 2013 katika wiki ya Hifadhi ya Jamii, Mfuko wa Pensheni wa PPF ulitunukiwa hati ya utambuzi kama Mfuko bora kwenye matumizi ya Mifumo ya habari. Hati hiyo ilitolewa na Mhe. Rais, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,kwa kuwa Mfuko bora katika Nyanja ya mifumo ya habari kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwenye kutoa huduma mbalimbali.
- Utoaji wa Mikopo ya SACCOS
Tunatoa mikopo hii kupitia SACCOS za wanachama wetu zilizopo kwenye maeneo yao ya kazi.
Mpaka sasa tumeshatoa zaidi ya Billioni 56 kwenye SACCOS 46
- Tuzo katika Utawala bora
- Hati safi kutoka kwa CAG kwa kuwa na mahesabu yaliyo safi
Tumewekeza kwenye ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwa ajili ya kuwauzia wanachama wetu.PPF imekuwa Mfuko wa kwanza kwa kuanzisha miradi ya nyumba za bei nafuu.
Tulijenga nyumba 580 Kiseke Mwanza na tuliziuza kwa bei nafuu ya kati ya shilingi millioni 16 mpaka million 33. Zoezi hili ni endelevu kwa mikoa mingine
- Fao la Elimu
LENGO
Katika Mpango mkakati wa Mfuko kwa kipindi cha miaka 3 (2013-2015) baadhi ya malengo ya Mfuko ni kama ifuatavyo:
- Thamani ya Mfuko ni kukua kutoka trillion 1.09 Desemba 2012 na kufikia trillion 2 ifikapo Desemba 2015
- Na Idadi ya wanachama kuongezeka kutoka wanachama 203,981 Desemba 2012 kufikia laki 4 Desemba 2015. Lengo kuongeza mara mbili thamani ya Mfuko
Mwisho kabisa ningependa kuwashukuru wanachama na wadau wote wa Mfuko kwa Mchango Mkubwa Mliotupa.
Hivyo tunaomba tuendelee kushirikiana kwa kuendelea kuwa wanachama wa PPF na wale ambao bado hamjajiunga na PPF tunaomba mjiunge ili muweze kuwa na uhakika wa maisha yenu ya sasa na baadaye.
Asanteni
Lulu Mengele
Meneja Uhusiano na Masoko
Mfuko wa Pensheni wa PPF
Simu: 0782 249994
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments