TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MAJERAHA YA SHEIKH PONDA ISSA PONDA
Dar es salaam 12/8/2013
Sheikh Ponda Issa Ponda (54) alipokelewa hapa taasisi ya ya tiba ya mifupa na upasuaji wa mishipa ya fahamu MOI jana tarehe 11/8/2013 saa 7.30 jioni akitokea hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kupokelewa alionekana akiwa na majeraha chini ya bega la mkono wa kulia lililokuwa limeshonwa mbele na nyuma madaktari wetu walifanya uchunguzi na kushauri afanyiwe
kipimo cha X-ray ili ubaini kama kuna mvunjiko kwenye sehemu ya jeraha tathimini ya madaktari baada ya kupata majibu ya X-ray ilionyesha alikuwa na mvunjiko bila mifupa kupishana vivyo hivyo kidonda hakikuwa katika hali nzuri licha ya tiba ya mwanzo na iliamuliwa afanyiwe upasuaji mpya ili kuzuia maambukizi kama kingeachwa hivyo.
KWA HIYO
1- kufwatana na tiba ya awali aliyopata ikiwa ni pamoja na kushonwa jeraha kabla kabla ya kufikishwa moi imekuwa vigumu kujua kama jeraha lilisababishwa na kitu gani
2- kipimo cha X-ray kilionyesha kwamba alikuwa amepata mvunjiko wa mfupa mkubwa wa bega bila mifupa kupishana
3- hivyo basi Sheikh Ponda Issa Ponda anaendelea n matibabu baada ya upasuaji.
Mkurugenzi Mtendaji
Taasisi ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu MOI
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments