[wanabidii] Kodi ya SIM-Card

Tuesday, August 27, 2013
Kikao cha 10 cha Bunge letu tukufu kinaanza leo. Bila shaka mojawapo ya mada zitazozungumziwa ni kodi ya 'line' za simu za mkononi iliyopitishwa na bunge hilo hapo nyuma.

Je, wanajukwaa, kuna mtu anajua matumizi ya pesa inayokatwa katika huduma mbalimbali kama vile maji na umeme kwenda EWURA inavyotumika? Kuna tetesi kuwa wapo watu humo hujilipa hadi Million 15 kwa mwezi! ni kwa kazi gani ya zaidi ya watumishi wa umma wengine? Kwa nini Serikali haidhibiti huko kabla ya kumkamua raia anayetegemea 'ku-bipu' ili apigiwe?

Mwenye data naomba nisaidie katika hili.

Tibu.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments