[wanabidii] KATIBA ISIMTAMBUE MUNGU WALA DINI

Wednesday, August 07, 2013

Ndugu zangu

Kwa muda mrefu serikali yetu imekuwa ikijitapa kwamba haina dini na kwamba nchi yetu iko huru mtu kuabudu kitu chochote hata mawe lakini yenyewe ikifanya tofauti na vile ambavyo inatakiwa iwe .

Kwa mfano tumeona wabunge ambao ni watunga sheria na wanaowakilisha makundi mbalimbali ya kijamii nchini wakiapa bungeni kwa kutumia vitabu vya dini zao , tumeona marais na mawaziri wakivaa mawazi yanayowakilisha dini Fulani wanapoenda kwenye shuguli zinazohusu dini hizo wakati wao ni viongozi wa Jamii ya watanzania .

Juzi na jana tumeona serikali hiyo hiyo kupitia viongozi wake wakitoa kauli zinazotatanisha kuhusu sikukuu za iddi na sikukuu za nane nane ambayo ni ya serikali wakati hiyo ya iddi ni ya kiislamu .

mimi naona ni wakati sasa kwa katiba yetu mpya kutamka wazi kuhusu masuala ya dini haswa hili la kutokumtambua mungu kwenye katiba na kutokuitambua dini yoyote lakini watu wapewe uhuru wa kuabudu wanachotaka ila inapofikia kitaifa basi taifa lisimame kama taifa bila ubaguzi wa aina yoyote .

ni matumaini yangu kwamba mjadala huu utakuwa mzuri kuhusu uwezekano wa kuiondoa dini kwenye katiba yetu .

kwenye nchi yetu kuna makundi mwengi ya kijamii ambayo hayana dini yoyote haswa maeneo ya kanda ya ziwa wengine wanadini lakini idadi yao ni ndogo wamekuwa wanatengwa au hawajadiliwi kwenye baadhi ya vitu vya kitaifa kama vile hawapo .


--
Find Jobs in Africa Jobs in Africa
International Job Opportunities International Job Opportunities
Jobs in Kenya Jobs in Kenya

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments