Wauaji wanafanya sherehe ya mauaji bila upinzani, majambazi wapora mchana kweupe bila mtu wa kuwazuia, mbaya zaidi hata wageni wanaokuja kutusaidia kutufundishia watoto wetu nao wanamwagiwa tindikali.
Haya yote yanatokea kwa kuwa Polisi wameacha majukumu yao ya kuwalinda raia na mali zao na badala yake wanatumia muda mwingi kupokea amri kutoka kwa viongozi wa CCM ili kuwabambikia Viongozi na Wanachama wa Chadema kesi za ugaidi!
Kwa kuwa hili la kuwambambikia Chadema kesi za UGAIDI limeshindikana, rudini kwenye jukumu lenu la USALAMA wa Raia ili msizidi kuumbuka kama mlivyoumbuka kwenye Kesi ya Dr Ulimboka!
0 Comments