[wanabidii] BIG RESULTS NOW au BIG DISASTERS NOW?

Monday, August 26, 2013
BIG RESULTS NOW au BIG DISASTERS NOW?

Sasa serikali imekuja na kauli mbiu mpya ya "MATOKEO MAKUBWA SASA" yaani kwa kimombo BIG RESULTS NOW

Kiuungwana tunaipongeza serikali na hizi jitihada za kutaka kuleta mabadiliko makubwa sasa japo kwa njia ya zima moto

Kwa mtazamo wangu hii kauli mbiu ni mwendelezo wa kauli mbiu nyingi zilizopita na kwa uchache sana nitoe hii moja ya ARI MPYA,NGUVU MPYA NA KASI MPYA(ANGUKA)

Kwanini tunapenda kufanya vitu vyenye kugharimu pesa za walipa kodi na hata pengine maisha yao kwa njia ya ZIMAMOTO?BIG RESULTS NOW kwa sasa ni wimbo kwa kila wizara na idara ya serikli

Huu si mpango maalum wenye lengo maalum kwa watu maalum?Ni kiasi gani cha pesa kimetengwa kwa utekelezaji wake?Je,uwazi wake upoje kwa watanzania?Tunaweza kushawishiwa kuwa si ukusanyaji wa awali wa pesa za kampeni za 2015 maana yale kama ya EPA yatakuwa magumu kwa sasa?

Tuje kwenye sekta ya elimu tu,zile shule zetu za UMMA(shule za kata)zimeandaliwa vipi na hii BIG RESULTS NOW?Kwao haitakuwa ni BIG DISASTERS NOW tokana na kulazimishwa kutekeleza kile kilichopo nje ya uwezo wao kimkakati na mazingira?

Tunahitaji BIG RESULTS NOW au QUALITY RESULTS NOW?Hayo matokeo makubwa ni hasi au chanya?Kwa aina gani ya watendaji na watekelezaji wa serikali?

Tunawezaji kuwa na BIG RESULTS NOW kwa wanavijiji wa NAMANYERE,KAZULAMIMBA,NAMTUMBA au KIPUMWIKO kwenye sekta ya kilimowakti bei za pembejeo badozipo juu?Wakati bado kilimo si tena uti wa mgongo tokana na matumizi ya jembe la mkono na kutegemea mvua za misimu?

Sipinganani na hii jitihada ya serikali ya MATOKEO MAKUBWA SASA ila hofu yangu ni ujumla wake kiutekelezwaji na hata maaandalizi yake duni.

BIG RESULTS NOW imepewa sura ya kisiasa zaidi na inasimamiwa nawanasiasa zaidi na tusubirimatokeo yaa kisiasa zaidi,ndio maana naendeleakusema na kuamini kuwa haitakuwa BIG RESULTS NOW bali BIG DISASTERS NOW.

TUTAFAKARI PAMOJA

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments