[Mabadiliko] Neno Fupi La Usiku Huu; Kwenye Jua Kuna Upendo Pia...!

Friday, August 16, 2013

Ndugu zangu,

Kwenye sura ya jua kuna ishara za upendo, ishara za mapenzi. Maana, jua linapowaka kuna mvuke unaotoka ardhini na kwenda juu angani. Na mvuke unapoganda, basi, ndipo matone ya maji yanapodondoka tena ardhini, ni mvua. Yaweza kuwa ya manyunyu, lakini ni mvua.

Naam, ni matone ya maji yanayoshuka ardhini yakiwa na mbawa na yenye furaha. Mvua hainyeshi kimya kimya, huja na sauti. Ni sauti ya furaha. Sauti iliyojaa upendo.

Hivyo, na vilivyo ardhini navyo hulipuka kwa furaha, maua hustawi na kuchanua kwa furaha.

Kondoo, mbuzi na hata kuku, nao hutoa sauti za furaha. Ah, ndege na vifaranga pia, navyo hutoa sauti. Vyote hivyo huja katika upendo, katika mapenzi.

Ni Neno Fupi La Usiku...
Maggid,

http://mjengwablog.com

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
 
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments