Hapa chini kuna articles mbili ambazo no ni habari zenye kipaumbele kwa siku ya leo, lakini imenifanya niweke articles zote mbili kwa pamoja kwa kuwa nimejiuliza maswali bila majibu. Inakuwaje Waachina ambao sote tunajua ndio wahitaji wakubwa wa pembe za ndovu wanapkamatwa hapa TZ kesi zao huishia kimya kimya? Wakati Biashara ya pembe za ndovu inazidi kuliumiza taifa letu, ndivyo biashara ya dawa za kulevya inaliumiza taifa la China. Tofauti na sisi, China imeweka sheria kali na sheria ya dawa za kulevya imepewa kipaumbele sana na adhabu yake ni kifo bila mjadala. Pengine ni wakati mwafaka sasa kwa Tanzania kuweka adhabu ya kifo bila mjadala kwa watakaopatikana na hatia ya kuua tembo au faru kwa ajili ya pembe. Akikamatwa Mchina, Mtanzania, Mkenya.... anyongwe hadi kufa.
Soma articles mbili tofauti hapo chini.Na Suleiman Msuya
WIZARA ya Maliasili na Utalii kupitia Idara ya Wanyamapori imesema zaidi ya tembo 475 wameuwawa na majangili kwa kipindi cha mwaka 2012/13 ambapo watuhumiwa 1215 walikamatwa kwa makosa mbalimbali.
Mkurugenzi wa Wanyamapori, Profesa Alexander Songoro pamoja na watuhumiwa hao pia jumla ya bunduki 85 na risasi 215 za aina mbalimbali zilikamwata na kesi 670 zilifunguliwa katika mahakama za hapa nchini, ambapo kesi 272 zimekamilika kwa washitakiwa 247 kulipa faini ya jumla ya Sh175,002,420 na washitakiwa 71 kupewa adhabu ya vifungo vya jumla ya miaka 99.
Alisema kesi 398 zenye jumla ya washitakiwa 897 bado zinaendelea katika mahakama mbalimbali nchini ambapo wanaamini kuwa zitakamilika hivi karibuni....... soma habari yote hapa
http://goldentz.blogspot.com/2013/07/ujangili-tanzania-tembo-475-mtanzania.html
TAARIFA MAALUM
Watanzania ambao idadi yao inaweza kupita mamia, wameshanyongwa nchini China kutokana na kupatikana na hatia ya kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.
Ripoti maalum ya madawa ya kulevya, iliyofanyiwa kazi na gazeti hili kwa kukusanya taarifa ndani ya nchi, Afrika Kusini na China kwenyewe, inaweka hadharani siri ya mamia ya Watanzania kunyongwa.
Katika ripoti hiyo, inaonesha kwamba mataifa ya Afrika Kusini na Uganda, yapo mstari wa mbele kuripoti taarifa za raia wao kunyongwa China lakini Tanzania imekuwa ikisuasua.
"Huu ukimya wa serikali yetu, unafanya wengi kukosa taarifa sahihi, matokeo yake wanajiingiza kwenye biashara hiyo haramu ambayo mtu akikamatwa tu China na akikutwa na hatia lazima anyongwe," alisema Joel Mabruki, mfanyabiashara wa nguo na simu kati ya Tanzania na China....soma story yake hapa
http://goldentz.blogspot.com/2013/07/watanzania-wanyongwa-kimya-kimya-china.html
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments