Jeshi la Magereza Tanzania Bara linapenda kuufahamisha Umma kwamba mnamo tarehe 23 Julai, 2013 Maafisa wanne ambao ni Mrakibu Msaidizi wa Magereza Joseph Kimaro, Sajenti Ketto Ramadhan, Koplo Silyvester Dionice na Wada Richard Barick wa Gereza Kiteto Mkoa wa Manyara walikamatwa na askari wa Kikosi cha Kuzuia Ujangili Kanda ya Kati wakiwa na gari la Jeshi la Magereza pamoja na silaha likiwa limepakia nyara za serikali.
Dereva wa gari hilo Sajenti Ketto Ramadhan alitoroka na kutelekeza gari hilo na Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu na maadili ya Jeshi la Magereza pamoja na sheria za uwindaji wa wanyama pori. Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Magereza limechukua hatua zifuatazo:-
Dereva wa gari hilo Sajenti Ketto Ramadhan alitoroka na kutelekeza gari hilo na Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu na maadili ya Jeshi la Magereza pamoja na sheria za uwindaji wa wanyama pori. Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Magereza limechukua hatua zifuatazo:-
i - Askari 3 waliohusika wamefukuzwa kazi kwa kosa la kwenda kinyume na maadili ya Jeshi la Magereza na watafikishwa Mahakamani baada ya upelelezi wa Polisi kukamilika.
ii - Afisa Mrakibu Msaidizi wa Magereza Joseph Kimaro amefunguliwa mashtaka ya kinidhamu na kusimamishwa kazi kwa kosa la kwenda kinyume na maadili ya Jeshi la Magereza hadi maamuzi ya Mamlaka ya kinidhamu inayomuhusu yeye (Disciplinary authority) itakapotoa maamuzi dhidi yake. Kwa sasa amezuiliwa Kituo cha Polisi Babati kusubiri kufikishwa Mahakamani upelelezi wa Polisi utakapokamilika.
iii - Mkuu wa Gereza Kiteto Mrakibu wa Magereza Ally Ramadhani Sauko kwa kutumia madaraka yake vibaya hivyo amevuliwa uongozi na kuhamishiwa Ofisi ya Mkuu wa Magereza Manyara, akisubiri maamuzi ya Mamlaka ya kinidhamu inayomuhusu yeye (Disciplinary authority) kufuatia mashtaka ya kinidhamu yaliyofunguliwa dhidi yake.
John Casmir Minja
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA
26 Juai 2013
Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/07/taarifa-ya-jeshi-la-magereza-kuhusu-askari-4-waliokamatwa-na-nyara-za-serikali.html#ixzz2aEOzjT9O
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments