[wanabidii] Shilingi 500/= sasa kuwa sarafu badala ya noti

Friday, July 05, 2013
KUTOKANA na kuchakaa haraka kwa noti ya shilingi 500 na kiwango chake kudumu kwenye mzunguko kwa miezi sita tu, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imesema inatarajia kubadili noti hiyo na kuwa ya sarafu.

Akizungumza na gazeti la Tanzania Daima jana kwenye viwanja vya maonesho ya kimataifa ya biashara, jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Fedha, Abdul Dollah, alisema mabadiliko hayo yatafanyika hivi karibuni na sarafu hiyo itadumu kwenye mzunguuko kwa zaidi ya miaka 20 huku ikiwa na ubora wake.

Dollah alitaja sababu nyingine ya uchakavu huo ni kutokana na noti hiyo kushikwa na watu wengi kwenye mzunguko huku baadhi yao wakishindwa kuzihifadhi vizuri: "Tofauti na noti nyingine kama vile zile za sh 5,000 na 10,000 hizi utakuta mara nyingi uchakavu wake si kama ule wa sh 500 kwa sababu noti hizi watumiaji wake wengi ni wale wenye akaunti benki."

Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2YAX32Odd

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments