TUME YA MABADILIKO YA KATIBA
__________
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
__________
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Jumanne, Julai 9, 2013
Tume ya Mabadiliko ya Katiba inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu kuwepo kwa Rasimu ya Katiba katika lugha ya Kiingereza iliyotolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ambayo inasambazwa kupitia njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii.
Rasimu hiyo ya Katiba katika lugha ya Kiingereza inatumika katika mikutano na makongamano mbalimbali yenye lengo la kujadili na kutoa maoni kuhusu Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume.
Tume ya Mabadiliko ya Katiba inapenda kuwafahamisha wananchi na wadau wengine kuwa Rasimu hiyo ya

Katiba katika lugha ya kiingereza iliyoandaliwa na LHRC haitoi tafsiri sahihi ya maudhui ya Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika lugha ya Kiswahili na hivyo kupotosha umma kuhusu maudhui ya Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume hivi karibuni.
Kwa msingi huo, Tume inawataka wananchi kuendelea kusoma na kutoa maoni kuhusu Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika lugha ya Kiswahili iliyozinduliwa tarehe 3 Juni, 2013 jijini Dar es Salaam.
Tume imeandaa Rasimu ya Katiba katika lugha ya Kiswahili ili kuwawezesha wananchi, ambao wengi wao wanajua kusoma na kuandika kwa lugha ya Kiswahili kuelewa maudhui ya Rasimu hiyo. Rasimu rasmi ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesambazwa kwa wananchi, taasisi, jumuiya na asasi mbalimbali na inapatikana katika tovuti ya Tume (www.katiba.go.tz).
Tume pia inapenda kuwafahamisha wananchi kuwa Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume haiuzwi na inapatikana katika ofisi za Tume zilizopo Dar es Salaam na Zanzibar.
Tume inawataka wadau wote wanaotaka kutafsiri Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume kuwasiliana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ina Wataalamu wa Unadishi wa Sheria (Legislative Drafters).
Mwisho.
Imetolewa na:
Bw. Assaa A. Rashid
Katibu,
Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
S.L.P. 1681,
Dar es Salaam

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments