[wanabidii] Ombi la msaada wa kupata kazi

Sunday, July 21, 2013
Salam sana wanabidii wenzangu,
Kwa kifupi mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 23. Nimemaliza masomo yangu ya chuo pale IFM mwaka huu ambapo nilikua nasomea kozi ya BBF( Bachelor Of Banking and Finance). Wakati huu tunasubiri majibu ambapo tunatarajia kukabidhiwa shahada zetu mwezi wa kumi na moja Mungu akipenda, nina ombi la msaada wa kupata connection itakayoniwezesha nami kupata kazi na taratibu kuanza kujipanga kimaisha. Nimejaribu kutuma maombi yangu sehemu mbali mbali bila mafanikio mpaka sasa na kinachonikwamisha kikubwa ni kutojuana na watu ambao wapo humu kwenye tasnia ya mabenki. Kuna baadhi ya wenzetu wachache ambao tulimaliza mitihani kama leo ni ijumaa then wakaripoti ma ofisini jumatatu. Kwa kweli kipindio hiki kimekua kigumu kidogo ukizingatia swala la kukaa nyumbani unakua kama ni mzigo fulani ndio maana natafuta sehem angalau nami niweze kuokoteza senti mbili tatu. Naomba kwa ndugu yangu yeyote ambae ni mfanyakazi wa benki au any financial institution au mwenye kujuana na mtu ambae yuko huko aweze kunisaidia kuni-link. Natarajia pia Mungu akiniajalia by november nifanye mitihani ya bodi (TIOB) na kuimalizia mwakani mwezi May ili niweze kupata cheti cha CPB (certified public banker).
Natanguliza shukrani za dhati na asanteni nyote!
Download the latest BlackBerry® applications from Zantel on www.zantel.com/zantelapps

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments