Madaktari wa umma wanaomiliki wa maduka ya dawa za binadamu wanatuhumiwa kuiba dawa na kuziuza, hali ambayo inasababisha watu kukosa imani na Serikali.
Kauli hizo zilitolewa juzi jioni wakati wajumbe wa Bodi ya Ushauri wa Huduma za Afya ya Mkoa wa Dodoma walipokutana pamoja na mambo mengine kujadiliana kuhusu uboreshaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).
Akichangia katika kikao hicho kilichoandaliwa na Mradi wa Kuhamasisha na Kuboresha Huduma za Afya (HPSS), Mkuu wa Wilaya, Lephy Gembe, aliwataka madaktari hao kutafakari na kuacha kumiliki maduka ya dawa: "Afadhali muende mkafungulie wilaya nyingine si mnapofanya kazi, mnatupa wakati mgumu sana…hili

linasababisha wananchi kukosa imani na Serikali yao,"alisema.
Gembe alisema hakuna ukaguzi wa dhati wa dawa za serikali katika maduka ya dawa binafsi, jambo ambalo linawafanya baadhi ya madaktari wasio waaminifu kuchukua dawa za serikali kupeleka katika maduka yao binafsi.
Meneja wa Kampeni wa HPSS, Phiona Chilunda, alizitaka halmashauri kununua vitabu vya kusaini viwili kwa ajili ya makabidhiano ya watu wanaopeleka maombi ya dawa kwenye mamlaka za Serikali: "Kumekuwa na mchezo wa kutupiana lawama za ucheleweshaji wa maombi ya dawa katika Bohari ya Dawa Nchini (MSD), kati viongozi wa Serikali za mitaa, wilaya na MSD wenyewe,"alisema.
Alisema ili kuondokana na kadhia hiyo ni vyema kukawa na vitabu hivyo ambacho kimoja kitakuwa kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya wanapopeleka maombi wilayani na cha wilaya kinachopeleka maombi MSD.

Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/07/madaktari-mnaomiliki-maduka-ya-dawa-mnatupa-wakati-mgumu-sana.html#ixzz2YRKqVRpF
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments