[Mabadiliko] Neno Fupi La Usiku; Mchezo Wa Vita Una Umri Wake..!

Friday, July 12, 2013
Ndugu zangu,

Utotoni mbali ya michezo mingine kuna tuliopenda kucheza ' Mchezo wa vita'. Kadri miaka ilivyoenda na umri kuongezeka kuna tulioelewa maana ya vita.

Binafsi nimeishi kumsikia kwa masikio yangu Amiri Jeshi Mkuu , Rais wa nchi akitangaza vita. Ni mwaka 1978. Ni kwenye Vita ya Kagera. Jioni ile nikiwa na miaka kumi na mbili tu niliiona tofauti ya siku hiyo na nyingine zote.

Nakumbuka usiku ule taa zilizimwa . Niliyaona magari ya kijeshi yalipita barabara ile ya Morocco, Kinondoni tulikokuwa tukiishi. Yalitokea kambi ya Lugalo.

Nakumbuka kumsikia Rais wa nchi, Julius Nyerere akitamka; " Vita si lelemama!" Katika umri wangu ule mdogo sikumwelewa Mwalimu Nyerere alimaanisha nini.

Naam, vita vya Kagera vilipomalizika nakumbuka kumsikia Julius Nyerere akitamka;

" Ndugu Wananchi, tuna miezi 18 ya kufunga mikanda". Julius Nyerere alimaanisha hali ngumu ya kiuchumi iliyokuwa ikija mbele yetu kama taifa.

Huenda Julius Nyerere alijua, kuwa ni zaidi ya miaka 18 migumu kiuchumi iliyo mbele yetu. Lakini, kama baba kwenye nyumba, ni vigumu kuiambia familia yako inayokutegemea, kuwa kuna miaka 18 mbele ya kuhemea chakula.

Leo naweza kabisa kuandika, kuwa sehemu ya matatizo yetu ya kiuchumi tuliyonayo sasa, yanatokana na makovu ya Vita Vya Kagera. Ni miaka 35 iliyopita.

Nahofia, kuwa hata sasa kuna miongoni mwetu wenye kutamani nchi iingie kwenye vurugu na hata vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kwamba wamechoka na amani tuliyo nayo.

Na wakati mwingine unafikiri, kuwa huenda kuna wenye kuaangalia sana filamu za kivita, sasa wanataka waone uhalisia wake.

Naamini, bado tuna nafasi ya kutatua matatizo mengi tuliyo nayo sasa, kwa njia za mazungumzo. Kwa njia za amani.

Naam, Vita si sawa na kucheza kombolela. Vita Si Lemama!

Ni Neno Fupi La Usiku.

Maggid,
Dar es Salaam.
0754 678 252
http://mjengwablog.com

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
 
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments