Ndugu zangu,
Leo ni mara ya kwanza nimekutana na Absalom tangu arudi kutoka matibabu yake kule Afrika Kusini.
Nimepata hisia mchanganyiko mara ile tulipoonana asubuhi ya leo; furaha na huzuni. Ni furaha ya kumwona tena Absalom akiwa hai, maana, yaliyomkuta yangeweza kabisa kumwacha kwenye mauti. Ni huzuni pia nikitafakari yale mateso aliyoyapata. Mateso ya kutekwa, kupigwa, kung'olewa kucha, meno, kukatwa kidole na hata kutobolewa jicho.
Tukiwa wawili tumepata fursa ya kuongea kwa kirefu sana. Tumekuwa pamoja na kuzungumza kwa zaidi ya saa mbili. Hakika, unapomwona Kibanda unaingiwa na hofu pia. Ni hofu ya wakati tulio nao, kuwa kuna Watanzania miongoni mwetu wenye kutenda ukatili dhidi ya wenzao. Unajiuliza, kwa nini tumefikia hapa?
Usiku Mwema.
Maggid
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments