Ndugu zangu,
Jana kunako saa sita mchana nilianza safari ya miguu nikiwa peke yangu. Nilitoka Ubalozi wa Sweden, Mtaa Mirambo na kuingia Shaabani Robert Street kuelekea Wizara Ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Na Watoto. Sikuwa na kamera wala simu yenye kamera. Nilikuwa ' Full Raia'!
Baada ya kumaliza shule ya Msingi Bunge , jengo linalofuatia ni la Msajili wa Vyama Vya Siasa. Linaitwa ' Nyumba Ya Demokrasia'. Nikakumbuka miaka ya 90 mwanzoni. Nilifika kwenye ofisi ya Bw. Liundi ambaye ndiye alikuwa Msajili wa Kwanza wa vyama vya siasa. Sikwenda kusajili chama, bali kuongea na Bw. Liundi. Nakumbuka Liundi alinikaribisha chai na tuliongea sana juu changamoto ya demokrasia katika nchi yetu. Sijui Mzee Liundi yuko wapi siku hizi.
Wakati nikiendelea na safari yangu ya miguu, basi, baada ya jengo la Msajili mbele kidogo ndipo ilipo Hazina. Na ukiwa hapo unaliona lango kuu yalipo makazi na ofisi ya Bwana Mkubwa Wa Nchi- JK. Na hapo nikakutana na ndugu zangu kwenye familia ya wanahabari; Boniface Makene na John Mapinduzi wakiwa na Mbunge Mstaafu Mzee Eliakim Simpasa. John na Boniface wako Ofisi ya Makamu wa Rais.
Tukaongea kidogo, na ilibaki kidogo nimkumbushe Mzee Simpasa juu ya ugomvi wake na wanahabari, enzi hizo akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki na Maadili. Maana, nakumbuka siku moja akiwa bungeni, Simpasa, alimwomba Spika amwamuru mwandishi wa habari, silikumbuki jina lake, aingie Bungeni na ajieleze mbele ya Bunge juu ya habari potofu aliyoiandika juu ya ' Bunge Tukufu'. Eliakim Simpasa alikuwa kama ' Dikteta' fulani hivi!
Naam, nilisita kumkumbusha Mzee Simpasa, maana, yawezekana mwandishi huyo alikuwa ni John Mapinduzi au Boniface Makene! Na leo hii wanatembea mitaani kama ndugu!
Good Morning!
Maggid Mjengwa
Dar es Salaam.
0754 678 252
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments